Nile
Mto wa Nile (pia: Naili; Kiarabu النيل an-nīl) ni mto mkubwa kwa upande wa Mashariki ya bara ka Afrika. Mara nyingi hutajwa kuwa pia mto mrefu kabisa duniani kushinda mto Amazonas. Kutoka Ziwa la Viktoria Nyanza hadi mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea Nile inavuka nchi za Uganda, Sudan na Misri kwa urefu wa 6,650 km.
Nchi za beseni ya mto wa Nile pamoja na tawimito | |
---|---|
Mto wa Nile | |
Jina: | an-Nil (Kiarabu) |
Mahali: | Africa ya kaskazini-mashariki |
Urefu: | 6650 km |
Chanzo: | Luvironza />mto wa chanzo Burundi |
Kimo cha chanzo: | 2.700 juu ya UB |
Mdomo: | Mediteranea kaskazini ya Kairo/Misri |
Kimo cha mdomo: | 0.00 m juu ya UB |
Tofauti ya kimo: | 2.700 m |
Tawimito ya kulia: | Sobat, Nile ya buluu (Abbai), Atbara |
Tawimto wa kushoto: | Bahr al-Ghazal |
Miji mikubwa mtoni (pamoja na vyanzo vyake): | Alexandria, Assuan, Atbara, Bahri, Fajum, Giza, Jinja, Juba, Kairo, Kampala, Khartum, Kigali, Kusti, Luxor, Malakal, Omdurman, Port Said, Rabak, Tanta |
Je inafaa kama njia ya maji? | ndani ya Misri |
Beseni ya Nile hukusanya maji ya eneo linalojumlisha 10% za eneo la Afrika yote au 3,349,000 km². Takriban watu milioni 250 hukalia beseni hiyo.
Jina
"Nile" au "Naili" ni umbo la Kiingereza la jina la mto kutokana na jina lililotumiwa na Wagiriki wa Kale "Neilos" (Νεῖλος). Haijulikani Wagrikiki walipata jina hili kwa njia gani lakini lilikuwa kawaida nje ya Misri. Wamisri wa Kale waliita mto huu kwa jina Ḥ'pī au iteru linalomaanisha "mto mkubwa". Wakopti walikuwa na jina la piaro lakini tangu utawala wa Kiroma jina la Kigiriki ilizidi kutumika na Waarabu waliendelea na jina la Kigiriki pia hivyo leo hii wananchi wanasema "an-nil".
Chanzo cha Nile
Nile ina vyanzo viwili ndivyo Nile yenyewe (inaitwa pia Nile nyeupe) inayotoka katika Ziwa Viktoria Nyanza na Nile ya buluu inayotoka katika Ziwa Tana. Majina haya ya "nyeupe" na "buluu" yana asili yao katika mji wa Khartoum ambako mito yote miwili inaunganika ilhali kila moja una rangi tofauti kutokana na udongo tofauti uliotia rangi yake kwenye maji yao.
Chemichemi za Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Viktoria Nyanza katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Kongo, Uganda na Kenya. Chanzo inayoanza mbali kabisa ni Mto wa Luvironza huko Burundi unaoingia katika Mto wa Kagera na kufika Ziwa Viktoria Nyanza.
Mkono mwingine wa Nile inaanza Ethiopia ikiitwa Abbai au Nile ya Buluu inatoka katika Ziwa Tana.
Hakuna mapatano kabisa Nile inaanza wapi. Kawaida ya waandisha Waingereza ni kuhesabu kuanzia Ziwa Viktoria; waandishi wa mataifa mengine huwa wanaweza kuita tayari mto wa Kagera kwa jina "Nile ya Kagera".
Majina ya Nile
Majina ya sehemu ya mto kuanzia Ziwa Viktoria hadi Khartoum ni kama yafuatayo:
- Nile ya Viktoria kuanzia Jinja inapotoka katika Ziwa Viktoria kwa 500 km hadi Ziwa Albert.
- Nile ya Albert kuanzia Ziwa Albert hadi mpaka wa Sudan
- ndani ya Sudan mto huitwa Bahr al-Jabal (mto wa mlimani) kuanzia mpaka wa Sudan hadi kupokea tawimto wa Bahr al-Ghazal
- kwa sababu ya rangi wakati wa mvua yake kutokana na udongo katika maji jina linakuwa Bahr al-Abyad kuanzia Bahr al-Ghazal hadi Khartoum
- kuanzia Khartoum jina ni pekee Bahr an-Nil (mto wa Nile) hadi mdomo wake wa delta kwenye Mediteranea.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nile kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |