Nenda kwa yaliyomo

Mlima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 17:10, 9 Februari 2010 na Kipala (majadiliano | michango) (Created page with 'thumb|300px|Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka [[Moshi (mji)|Moshi]] thumb|300px||[[Mount McKinley jimbo...')
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi
Mount McKinley jimboni Alaska (USA).

Mlima ni sehemu ya uso wa dunia iliyoinuka sana juu ya mazingira yake. Mifano katika Afrika ni Mlima Kilimanjaro au Mlima Kenya.

ilele na vilele

Kwa kawaida mlima huwa na kilele kimoja au zaidi; kwa mfano Kilimanjaro huwa na vilele vitatu vya Kibo, Mawenzi na Shira. Kama mlima ni pana sana vilele vyake vinaweza kuitwa mlima kila mmoja; kama mwiinuko fulani hutazamiwa kama mlima wa pekee au kama kilele kimojawapo hutegemea nan uzoefu. Wakati mwingine Kibo hutajwa kama "mlima" si kama kilele cha Kilimanjaro pekee halafu kwa maanau huu Kilimanjaro si mlima mmoja bali safu ndogo ya milima.

Milima mikubwa, milima midogo

Kama mlima unatazamiwa kama mrefu au la hutegemea mazingira yake. Katika nchi tambarare kabisa hata miinuko midogo ya mita 100 inaweza kuitwa "mlima". Katika eneo penye milima mingi na mirefu mwiinuko wa mita 1000 mara nyingi hukubaliwa kama mlima kwa sabau ni mdogo kulingana na milima mikubwa.

Lugha nyingi zinatofautisha kati ya milima mikubwa na midogo au vilima kwa mfano Kiingereza kwa maneno kama "mountain" na "hill". Lakini hata hapa hutegemea mazingira kama sehemu fulani huitwa hill au mountain. Uingereza huwa na sheria inayoita kila sehemu juu ya mita 600 "mlima".

Urefu wa mlima hutajwa kitaalamu kwa "mita juu ya uwiano wa bahari". Hata hivyo mlima unaweza kuonekana mdogo kiasi kama mazingira yake ni vyanda za juu na mwiinuko wake juu ya nyada za juu si mrefu sana; kinyume chake hata mlima mdogo kiasi unaweza kuonekana mkubwa kabisa kama mazingira yeka ni yote tambarare karibu na uwiano wa bahari.

Milima na maisha

Milima huwa muhimu kwa ekolojia ya uhai na maisha ya kibinadamu kwa sababu milima ni mahli pa mvua nyingi kushinda mazingira. Mito mingi duniani inaanza milima na hupeleka maji kutoka huko kwenda tambarare na mabonde.

Kuzaliwa na kupotea kwa milima

Milima huwa na historia inayoweza kutazamiwa kama maisha ya mlima. Milima hutokea kutokana na miendo ndani ya ganda la dunia.

Mabamba ya gandunia husukumana na kusababisha kukunja kwa sehemu fulani. Milima kama Himalaya katika Asia, Alpi za Ulaya au Atlas ya Afrika ya Kaskazini ilitokea hivyo. Miendo ya gandunia husababisha pia kutokea kwa milima baharini inayoweza kutokea juu ya uso wa maji kama visiwa. Milima iliyotokea kutokana na kukunjwa mara nyingi huonekana kama safu ndefu ya milima.

Njia nyingine ya kutokea kwa milima ni volkeno. Hapa magma (mwamba moto ulioyeyuka) inapanda kutoka koti ya dunia inakuta njia kupitia nafasi katika ganda la dunia na kufika usoni kwa umbo la lava. Hapa lava inaganda kuwa mwamba imara. Kama akiba ya magma chini ya volkeno ni kubwa inaendelea kupanda juu na kutoka kwenye kasoko ya volkeno. Inapanda juu ya lava iliyoganda tayari na kwa njia hii volkeno inazidi kukua.

Volkeno kubwa Afrika ni Kilimanjaro.

Baada ya kutokea milima inaendelea kuwa midogo polepole kutokana na miamba kuavunjika na kusagwa kwa njia ya mmomonyoko . Athira zinazosababisha mmomonyoko ni hasa toafuti za halijoti pamoja na maji, upepo na barafu.

Milima mirefu duniani

Mlima mrefu unaojulikana kabisa uko nje ya dunia kwenye sayari Mirihi unaitwa Olympus Mons na kuwa na urefu wa kilomita 27.

Mlima mrefu juu ya uso wa dunia huitwa Mount Everest (8,848m) uko mpakana wa nchin Nepal na Tibet katika Asia. Lakini mlima mrefu kabisa ni Mauna Kea katika fungovisiwa ya Hawaii. Unaonekana kama mlima mrefu wa Hawaii unaofikia mita 4,214 juu ya UB lakini ukitazamiwa kutoka chanzo chake unapoanza kuinuliwa juu ya mazingira yake chini ya bahari kilele chake kipo mita 10,205 mita juu ya mazingira tambarare yaliyoko chini ya bahari.

Milima mirefu ya bara ni kama zifuatazo:


Marejeo


Wikimedia Commons ina media kuhusu: