Attaullah Khan Esakhelvi
Attaullah Khan Niazi (kwa Kipanjabi: عطااللہ خان نیازی; anajulikana kama Attahullah Khan Esakhelvi, pia anajulikana kama Lala, maana yake "kaka mkubwa" kwa Kipashto na Kipanjabi; amezaliwa 19 Agosti 1951) ni mwanamuziki wa Pakistan kutoka Isakhel, Mianwali, Punjab.[1]
Attaullah Khan Niazi | |
---|---|
Amezaliwa | Attaullah Khan Esakhelvi Niazi 19 Agosti 1951 (Miaka 69) Mianwali, Punjab, Pakistan |
Kazi yake | Mwimbaji, Mwigizaji, Mwandishi |
Miaka ya kazi | 1971 – 2019 |
Serikali ya Pakistan ilimtunuku Sitara-e-Imtiaz mnamo 23 Machi 2019 na pia alipata Tuzo ya umashuhuri ya Utendaji mnamo 1991. Ana uhusiano na Denzel Washington na anaandika nyimbo zake zote mwenyewe.
Mnamo 2011 alionekana katika tamasha la Coke Studio (msimu wa 4) na kuimba nyimbo 3 amabazo ni: Ni Oothaan Waale, Baa Baa Blacksheep na Pyaar Naal. Mnamo Septemba 2017 alionekana katika Coke Studio (msimu wa 10) mara ya pili na kuimba Sab Maya Hai na sauti yake ya mapenzi ya jadi.
Maisha ya awali
haririEsakhelvi alizaliwa huko Esa Kheil, Mianwali, mkoa wa Punjab, Pakistan kama Attaullah Khan Niazi. Niazi ni kabila lenye watu wengi wa Pashtun wenyeji wa mkoa uliokithiri wa kaskazini-magharibi mwa Punjab Pakistan na maeneo ya mashariki mwa Afghanistan. Attaullah alikua anapenda muziki akiwa mtoto, lakini muziki ulikatazwa kabisa nyumbani kwake.[2][3] Licha ya kizuizi kwenye muziki nyumbani kwake, Attaullah alitafuta kwa siri kujifunza zaidi juu ya muziki.[2] Mwalimu wake wa shule alimfundisha nyimbo za Mohammed Rafi na Mukesh na kumwambia asiache kuimba. Attaullah alijaribu kuelezea mapenzi yake ya muziki kwa wazazi wake na kuwashawishi wamuache aimbe, lakini walimkataza kuendelea kuimba.[2] Akiwa amekata tamaa, Attaullah aliondoka nyumbani akiwa na umri wa miaka 18.[2] Alisafiri sana ndani ya Pakistan na akajikimu kwa kufanya kazi kutoka Mianwali. Yeye ni maarufu zaidi katika maeneo ya vijijini ya Pakistan na nchi zingine ulimwenguni.
Kazi katika muziki
haririEsakhelvi aliendelea na mafunzo baada ya kutoka nyumbani kwa wazazi wake na mara nyingi alijirekodi kwenye kanda za kaseti ambazo baadaye alisambaza.[2]
Mnamo 1972, Esakhelvi alialikwa kutumbuiza kwenye Redio Pakistan, Bahawalpur. Mwaka huo huo, alitumbuiza kwenye tamasha huko Mianwali.[4] Esakhelvi alitumbuiza kwenye kipindi cha televisheni Neelam Ghar mnamo 1973.
Alialikwa na kampuni huko Faisalabad kurekodi nyimbo za kitamaduni katika studio yao na kurekodi albamu nne katika kipindi kimoja cha kurekodi.[2] Albamu hizo zilitolewa mwishoni mwa 1977 na zikawa na mauzo zaidi kitaifa.[2]
Mnamo 1980, Esakhelvi alitumbuiza Uingereza kwa mara ya kwanza. Ilikuwa pia tamasha lake la kwanza nje ya nchi. Albamu zake mwishowe zilitolewa Uingereza chini ya maandiko anuwai, pamoja na Hi-tech, OSA na Moviebox.
Amewatumbuiza Na`at na Kalaam wa washairi mashuhuri wa Sufi, kama vile Saian Maluk wa Mian Muhammad Bakhsh na Keey Bay Dardan Sang Yaree wa Bulleh Shah. Aliimba pia wimbo wa Sadiq (mshairi mashuhuri wa saraiki).
Attaullah Khan alitembelea India mnamo 2014. Times of India iliandika: "Tamasha la Sufi, Ibaadat, lililoandaliwa kwa kushirikiana na Navbharat Times, lilifanyika hivi karibuni huko Purana Quila katika mji mkuu. Mwimbaji huyu wa Pakistani Attaullah Khan alitumbuiza kwa mara ya kwanza huko Delhi huko hafla hii. Khan aliimba wimbo wake wa Achha Sila Diya Tune Mere Pyaar Ka, na nyimbo zingine za Sufi za Pakistani kwa watazamaji.Tamasha hilo liliandaliwa na kikundi cha AAS, NGO ambayo inafanya kazi ya kueneza uelewa juu ya saratani ya kizazi kati ya wanawake na njia za kuizuia. na tamasha hili liliandaliwa kueneza ujumbe huo."[5]
Maisha binafsi
haririAttaullah Khan anatoka wilaya ya Mianwali na mji wake ni Esakhel. Alipata elimu yake ya mapema kutoka kwa Esakhel. Kijadi anachukuliwa kama msanii wa Chipunjabi.
Attaullah alihamia Lahore baada ya kuwa mwanamuziki mtaalamu anayecheza katika Punjabi, kiurdu na Kiingereza. Ameolewa mara nne na ana watoto wanne. Binti yake Laraib Atta ni msanii wa kitaalam wa VFX ambaye amewahi kufanya kazi kwa filamu kadhaa za Hollywood.[6][7] Mwanawe Sanwal Esakhelvi pia anaendelea na taaluma ya muziki,[8] wakati mtoto mwingine wa kiume, Bilawal, ni mwigizaji na mkurugenzi anayeishi London,[9] mbali na kuwa mwanamuziki.[10]
Marejeo
hariri- ↑ "Atta Ullah Eesakhelvi and the Cassette Revolution". All Things Pakistan. 2008-11-22. Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 "https://web.archive.org/web/20110810074729/http://www.ink-on-the-web.com/2011/06/22/" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-10. Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
{{cite web}}
: External link in
(help)|title=
- ↑ "Attaullah Khan Esakhelvi". Pakpedia | Pakistan's Biggest Online Encyclopedia (kwa American English). 2017-06-05. Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
- ↑ "Attaullah Khan Esakhelvi - A Pakistani Legend life History | The News Track - Part 1". web.archive.org. 2013-07-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-07-10. Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
- ↑ "Pakistani folk singer Attaullah Khan performed during a Sufi concert at Purana Quila in Delhi - Times of India". The Times of India (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
- ↑ Mehreen Hasan (2015-09-04). "I hope to work on projects in Pakistan, says Hollywood VFX artist Laraib Atta". DAWN.COM (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
- ↑ "Meet Laraib Atta: Pakistani visual effects prodigy making waves in Hollywood". The Express Tribune (kwa Kiingereza). 2015-08-31. Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
- ↑ "Attaullah Khan Esakhelvi on what makes him the common man's artist". The Express Tribune (kwa Kiingereza). 2016-04-06. Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
- ↑ "I feel the pressure every time I look at the keyboard or the harmonium: Sanwal Esakhelvi | HUM TV - Watch Dramas Online" (kwa American English). 2018-04-23. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-24. Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
- ↑ "Bilawal Atta: Photographer, Camera Operator and Writer / Director - London, UK". StarNow (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-12. Iliwekwa mnamo 2021-04-12.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Attaullah Khan Esakhelvi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |