Doris Lessing
Doris May Lessing (amezaliwa 22 Oktoba 1919) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Uingereza akiwa amezaliwa nchini Uajemi. Aliandika pia chini ya lakabu ya Jane Somers. Mwaka wa 2007 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Lessing amezaliwa kwa jina la Doris May Tayler nchini Uajemi tarehe 22 Oktoba, 1919. Wazazi wake walikuwa Alfred Tayler aliyefanya kazi huko Uajemi kwa Benki ya Ufalme wa Uajemi ("Imperial Bank of Persia") na Emily Maude Tayler. Mwaka wa 1925, familia walihamia nchi ya Zimbabwe (au Rodesia Kaskazini ilivyoitwa wakati huo). Baada ya kuhitimu shule, Lessing alihamia mji wa Salisbury kufanya kazi kama opereta wa simu. Aliolewa mara ya kwanza na Frank Wisdom na kuzaa watoto wawili. Wakapeana talaka mwaka wa 1943. Ndoa ya pili, Lessing aliifunga na Gottfried Lessing; walikuwa na mtoto mmoja kabla ya kutengana tena mwaka wa 1949. Alikuwa ameanza kuandika, hasa kuhusu mambo ya kisiasa dhidi ya ubaguzi wa rangi. Kwa hiyo alikataliwa kuishi Zimbabwe, akalazimishwa kuhama. Tangu mwaka wa 1949 ameishi mjini London, Uingereza.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mshindi wa Tuzo ya Nobel bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Doris Lessing kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |