Eva Green
Eva Green | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Green akiwa katika ugawaji wa Tuzo za BAFTA huko mjini London, kunako mwezi wa Februari wa mwaka wa 2007. | |||||||
Amezaliwa | Eva Gaëlle Green 5 Julai 1980 Paris, Ufaransa | ||||||
Kazi yake | Mwigizaji, Mwanamitindo | ||||||
Miaka ya kazi | 2003–hadi leo | ||||||
|
Eva Gaëlle Green (amezaliwa tar. 5 Julai 1980) ni mwigizaji filamu wa Kifaransa. Eva, alikulia mjini Paris na kuishi katika moja ya sehemu za mjini London. Eva, alishawahi kuelezewa na gazeti la Vogue kuwa yeye ana "mwonekano wa kiuaji, ana akili nyingi na pia mnyenyekevu", na pia ana sura nzuti ya kuvutia.[1]
Huyu ni binti wa mwigizaji Bi. Marlène Jobert. Hapo awali, Green alikuwa akitumbuiza katika makumbi kadhaa kabla ya kushiriki kwa mara yake ya kwanza katika filamu ya The Dreamers (2003), ambayo imezua mabishano kadhaa juu ya mwanama huyu kuonekana akiwa mtupu katika picha zake nyingi alizofanya humo.
Alijipatia umaarufu wake mkubwa baada ya kucheza katika filamu ya Kingdom of Heaven (2005), na vilevile kucheza katika filamu ya 2006 ya James Bond maarufu kama Casino Royale, ambayo imempatia tuzo ya BAFTA. Pia amefanya shughuli za kimitindo na makampuni kadha wa kadha.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Filamu | Jina alilotumia | Maelezo na Tuzo |
---|---|---|---|
2003 | The Dreamers | Isabelle | Ameteuliwa kama Mwigizaji Bora wa Ulaya na European Film Awards |
2004 | Arsène Lupin | Clarisse de Dreux-Soubise | |
2005 | Kingdom of Heaven | Sibylla | |
2006 | Casino Royale | Vesper Lynd | Ameshinda - BAFTA Tuzo ya Nyota Chipukizi Ameshanda - Empire Award kwa kuwa mwigizaji bora wa kike - chipukizir Nominated - Saturn Award for Best Supporting Actress Nominated - National Movie Awards for Best Best Performance by a Female Nominated - Irish Film and Television Awards for Best International Actress |
2007 | The Golden Compass | Serafina Pekkala | |
2008 | Franklyn | Emilia | |
2009 | Cracks | Miss G | bado inatengenezwa tangazo zake |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Eva Green", The Independent Magazine, 14 Aprili 2007.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Eva Green kwenye Internet Movie Database
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eva Green kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |