Homa ya matumbo
Homa ya matumbo (kwa Kiingereza typhoid fever) husababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella Typhi. Ugonjwa huu huambukizwa kwa mtu kula au kunywa chakula au maji yaliyo na kinyesi cha mtu aliyeambukizwa.[1] Bakteria hao hutoboa na kunyonya chakula kwenye matumbo ya binadamu.
Dalili
[hariri | hariri chanzo]- Homa kali
- Kutoka kwa jasho jingi
- Kuharisha (bila ya kutoa damu)
- Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.
Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa huwa na hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.
Katika wiki ya kwanza:
- Joto la mwili huongezeka
- Kichwa huuma
- Kukohoa
- Damu kutoka puani, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
- Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea
Katika wiki ya pili:
- Homa huongezeka
- Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
- Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
- Kuharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
- Kutapika kwa mgonjwa
- Ini linavimba
- Homa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.
Wiki ya tatu:
- Matumbo hutoa damu
- Matumbo hutoboka
Wiki ya tatu ikimalizika, homa huanza`kutulia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.
Matibabu
[hariri | hariri chanzo]Mara nyingi, homa ya matumbo haiui binadamu. Dawa kama ampicillin, chloramphenicol, trimethoprim-sulfamethoxazole, amoxicillin and ciprofloxacin hutumika kutibu wagonjwa.
Hatua za kuzuia kupata homa hii
[hariri | hariri chanzo]- Usafi wa mazingira na wa nafsi ni hatua bora ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
- Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hiyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
- Homa hii huweza kuenea kwenye mazingira ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kinga bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
- Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majina Typhim Vi iliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherix iliyotengenezwa na GlaxoSmithKline.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 2004-2005, janga la homa ya matumbo lilizuka katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoathiri watu 42,000 na kuua watu 214 (kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani).
Waathiriwa maarufu
[hariri | hariri chanzo]- Mary Mallon, aliyejulikana kama Typhoid Mary.
- Louisa May Alcott, mwandishi wa Little Women.
- Charles Darwin, mwanasayansi, aliathirika pindi alipoenda nchini Chile mnamo 1835.
- Eugenia Tadolini, alikufa mjini Paris mnamo 1872.
- William Wallace Lincoln, mtoto wa tatu wa Abraham Lincoln, rais wa 16 wa Marekani, pamoja na Mary Todd Lincoln, walifariki kutokana na maradhi haya mnamo 20 Februari 1862.
- Wilbur Wright, alikufa mnamo 30 Mei 1912 baada ya kuugua homa hii.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Giannella RA (1996). "Salmonella". Baron's Medical Microbiology (Baron S et al., eds.) (tol. la 4th). Univ of Texas Medical Branch. ISBN 0-9631172-1-1.
Kusoma zaidi
[hariri | hariri chanzo]- Easmon C (2005-04-01). "Typhoid fever and paratyphoid fever". Travel Health. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-13. Iliwekwa mnamo 2008-10-05.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Harrison NG. Walter Reed and Typhoid Fever, 1897–1911. Univ of Virgina. Retrieved on 2008-10-05.
- Nicolson publisher=BBC News, Stuart (2008-06-26). "Typhoid left city (Aberdeen) 'under siege'". Iliwekwa mnamo 2008-10-05.
{{cite news}}
: Missing pipe in:|last=
(help) - O'Hara C (2006-01-26). "Typhoid Fever Led To The Fall Of Athens". Elsevier. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-30. Iliwekwa mnamo 2008-10-05.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Homa ya matumbo kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |