Nenda kwa yaliyomo

Maambukizi ya virusi vya papilloma vya binadamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maambukizi ya virusi vya papilloma vya binadamu
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuMagonjwa ya kuambukiza, Jinakolojia, Onkolojia
DaliliHakuna, uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi[1][2]
VisababishiVirusi vya papilloma ya binadamu husambaa kwa njia ya mgusano wa moja kwa moja[3][4]
KingaChanjo za HPV, kutofanya ngono, mwenza mmoja maishani, kondomu[5][6]
Idadi ya utokeaji wakeWatu walio wengi wameambukizwa na HPV wakati fulani katika maisha yao[3]

Maambukizi ya virusi vya papilloma ya binadamu (HPV infection) ni maambukizi yanayosababishwa na virusi vya papilloma ya binadamu.[4]

Takribani asilimia 90 ya maambukizi hayo hayasababishi dalili zozote na hutoweka yenyewe ndani ya miaka miwili.[1] Hata hivyo, katika baadhi ya visa, maambukizi huendelea na kupelekea uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi au vidonda vya awali vya saratani.[2] Vidonda hivi, kulingana na eneo lililoathiriwa, huongeza hatari ya saratani ya mlango wa uzazi kwa wanawake, uke (vagina), midomo ya uke (vulva), uume, mkundu, kinywa au koo.[1][2] Karibu saratani yote ya mlango wa uzazi kwa wanawake inatokana na HPV; ziko aina mbili, yaani HPV16 na HPV18, hizi huchangia asilimia 70% ya maambukizi.[1][7] Kati ya asilimia 60% na 90% ya saratani zingine zilizoorodheshwa hapo juu pia zinahusishwa moja kwa moja na maambukizi ya HPV.[7] HPV6 na HPV11 ni visababishi ambavyo hutokea mara kwa mara vya uvimbe mdogo wa nyama kwenye sehemu za siri na papilomatosisi ya koo (laryngeal papillomatosis).[1]

Maambukizi ya HPV husababishwa na virusi vya papilloma ya binadamu, ambayo ni aina ya kirusi cha DNA kutoka kwenye jamii ya virusi vya papilloma.[8] Zaidi ya aina 170 zimeelezewa.[8] Zaidi ya aina 40 zinaweza kuenea kwa njia ya kujamiiana na kuambukiza mkundu na sehemu za siri.[3] Sababu hatarishi kwa maambukizi ya mara kwa mara kwa njia ya ngono hujumuisha kuanza kujamiiana kwa mara ya kwanza wakati mtu akiwa na umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi wa kingono, uvutaji sigara, na utendaji dhaifu wa kingamwili.[1] Kwa kawaida aina hizi huenezwa kwa mgusano endelevu wa moja kwa moja wa ngozi hadi ngozi, huku kufanya mapenzi kwa njia ya uke na mkundu zikiwa ndizo njia zinazojulikana zaidi kuleta maambukizi. [3] Pia, maambukizi ya HPV yanaweza kuenea kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito.[9] Hakuna ushahidi kwamba HPV inaweza kuenea kupitia vitu vya kawaida kama vile vyoo vya kukalia,[10] japo aina zinazosababisha uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi zinaweza kuenea kupitia maeneo kama vile sakafu.[11] Mtu anaweza kuambukizwa na aina moja au zaidi ya HPV.[9] HPV inajulikana kuathiri wanadamu pekee.[4][12]

Chanjo za HPV zinaweza kuzuia aina ya maambukizi ya kawaida.[3] Chanjo inapaswa kutumika kabla ya kuanza kujihusisha na mapenzi ili kuleta ufanisi zaidi, na kwa hivyo inapendekezwa kutumika kati ya umri wa miaka 9 hadi 13.[1] Matumizi ya mara kwa mara ya kondomu ya kiume yanaweza kupunguza maambukizi ya HPV kwa wanawake kwa takribani asilimia 70, ingawa maeneo ambayo hayajafunikwa (na kondomu) yanaweza kuambukiza eneo la nje la uke.[5][6] Kujizuia kufanya ngono au kuwa na mwenzi mmoja tu maishani, kunaweza kupunguza maambukizi ya HPV ya sehemu za siri.[5] Uchunguzi wa saratani ya mlango wa uzazi wa wanawake, kwa njia ya uchunguzi wa Papanicolaou ("pap smear"), au uchunguzi wa seviksi baada ya kupaka asidi asetiki (acetic acid), unaweza kugundua saratani ya mapema na seli zisizo za kawaida ambazo zinaweza kuibuka na kuwa saratani.[1] Uchunguzi hupelekea matibabu ya mapema ambayo huleta matokeo bora.[1] Uchunguzi umepunguza idadi ya visa vya maambukizi na idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya mlango wa uzazi wa wanawake.[13] Uvimbe mdogo wa nyama kwenye ngozi unaweza kuondolewa kwa njia ya kugandisha (freezing).[4]

Karibu watu wote katika maisha, wamewahi kupata maambukizi ya HPV.[3] HPV ni moja ya aina ya kawaida zaidi ya maradhi ya zinaa (STI) ulimwenguni.[5] Mnamo mwaka wa 2018, inakadiriwa kuripotiwa visa 569,000 vya saratani ya mlango wa uzazi, pamoja na vifo 311,000.[14] Takribani asilimia 85 ya saratani hizi za mlango wa uzazi zilitokea katika nchi zenye kipato cha chini na kipato cha katikati.[1] Nchini Marekani, takribani visa 30,700 vya saratani zinazotokana na HPV hutokea kila mwaka.[15] Kwa makadirio, asilimia 1 ya watu wazima wanaojamiiana, wana vidonda (warts) vinavyoota sehemu za siri.[9] Visa vya vidonda kwenye ngozi (skin warts) vimeelezewa tangu zamani za Ugiriki ya Kale, ikiwa ni kweli kwamba vidonda hivi husababishwa na virusi na ilibainika mnamo mwaka wa 1907.[16]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 "Human papillomavirus (HPV) and cervical cancer". WHO. Juni 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 Ljubojevic S, Skerlev M (2014). "HPV-associated diseases". Clinics in Dermatology. 32 (2): 227–34. doi:10.1016/j.clindermatol.2013.08.007. PMID 24559558.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 "What is HPV?". CDC. 28 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 Milner, Danny A. (2015). Diagnostic Pathology: Infectious Diseases. Elsevier Health Sciences. uk. 40. ISBN 9780323400374. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Septemba 2017.
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 Nakra, Natasha A.; Blumberg, Dean A. (2022). "16. Human Papillomavirus infections and prevention". Katika Jong, Elaine C.; Stevens, Dennis L. (whr.). Netter's Infectious Diseases (kwa Kiingereza) (tol. la 2nd). Philadelphia: Elsevier. ku. 71–74. ISBN 978-0-323-71159-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 2 Oktoba 2023.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 "Fact Sheet for Public Health Personnel | Condom Effectiveness | CDC". www.cdc.gov. 25 Machi 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Mei 2017. Iliwekwa mnamo 1 Mei 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 "The Link Between HPV and Cancer". CDC. Septemba 30, 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Novemba 2015. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. 8.0 8.1 Bzhalava D, Guan P, Franceschi S, Dillner J, Clifford G (Oktoba 2013). "A systematic review of the prevalence of mucosal and cutaneous human papillomavirus types". Virology. 445 (1–2): 224–31. doi:10.1016/j.virol.2013.07.015. PMID 23928291.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. 9.0 9.1 9.2 "Human Papillomavirus (HPV) Questions and Answers". CDC. 28 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "5 Things You Might Not Know About Human Papillomavirus". CDC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 22 Mei 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Human Papilloma Virus (HPV)" (PDF). WRHA. 18 Novemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 26 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Pink Book (Human Papillomavirus)" (PDF). CDC.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 21 Machi 2017. Iliwekwa mnamo 18 Aprili 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. Sawaya GF, Kulasingam S, Denberg TD, Qaseem A (Juni 2015). "Cervical Cancer Screening in Average-Risk Women: Best Practice Advice From the Clinical Guidelines Committee of the American College of Physicians". Annals of Internal Medicine. 162 (12): 851–9. doi:10.7326/M14-2426. PMID 25928075.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "Global Cancer Observatory: International Agency for Research on Cancer" (PDF). IARC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 11 Oktoba 2018. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. Viens LJ, Henley SJ, Watson M, Markowitz LE, Thomas CC, Thompson TD, na wenz. (Julai 2016). "Human Papillomavirus-Associated Cancers - United States, 2008-2012". MMWR. Morbidity and Mortality Weekly Report. 65 (26): 661–6. doi:10.15585/mmwr.mm6526a1. PMID 27387669.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. Tyring, Stephen; Moore, Angela Yen; Lupi, Omar (2016). Mucocutaneous Manifestations of Viral Diseases: An Illustrated Guide to Diagnosis and Management (tol. la 2nd). CRC Press. uk. 207. ISBN 9781420073133. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 3 Agosti 2020.