Mafuta (chakula)
Mafuta au shahamu ni sehemu za chakula pamoja na wanga, protini na vitamini. Neno "fati" (kutoka Kiing. fat) afadhali lizuiwe. Vyakula vilivyo na mafuta mengi ni k.m. maparachichi, karanga, makorosho, mbegu kama alizeti na siagi.
Vyakula hivi humsaidia mtu kwa kumpatia joto hasa wakati wa baridi, pia huchangia katika uzalishaji wa nishati na nguvu kwa ajili ya mwili na pia hufanya kazi mbalimbali katika mmeng'enyo wa chakula tumboni.
Athari za mafuta mengi mwilini
[hariri | hariri chanzo]Vyakula hivi huhitajika kwa asilimia chache sana ndani ya mwili. Vyakula vya mafuta vikizidi mwilini huwa na madhara kama kuziba mishipa na kusababisha ugonjwa huitwao shinikizo la damu au maarufu kama presha. Ugonjwa huu hutokana na mafuta kuganda moyoni na kusababisha moyo kushindwa kusukuma damu ipasavyo.
Pamoja na hayo, huenda ukawanda kupindukia ukawa mnene mno. Hili likifanyika, wafaa ufanye mazoezi na ule chakula kisicho na ufuta mwingi. Hata hivyo kuwanda si ishara kwamba umekula sana, maana kuwa watu ambao hunenepa maana ile hali iko katika nasaba yao (hereditary genes).
Kupunguza mafuta mwilini
[hariri | hariri chanzo]Ni vyema kufanya mazoezi kila siku, kula vitu visivyo na ufuta kupindukia na kuunywa maji mengi maana maji husaidia katika metaboli.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- https://www.webmd.com/diet/obesity/features/are-you-fated-be-fat Hereditary Obesity
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mafuta (chakula) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |