Nenda kwa yaliyomo

Mataifa ya G20 ya viwanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mataifa ya G20 ya viwanda
Nchi zenye rangi ya buluu nzito ni wanachama wa G-20; zenye rangi ya samawati ni wanachama wa Umoja wa Ulaya wasio na uwakilishi wa pekee.
Limeanzishwa1989*
Region served
WWW:
Membership
01.Bendera ya Argentina Argentina
02.Bendera ya Australia Australia
03. Marekani
04.Bendera ya Kanada Kanada
05.Bendera ya Ufaransa Ufaransa
06.Bendera ya Italia Italy
07.Bendera ya Mexiko Meksiko
08.Bendera ya Urusi Urusi
09. China’PR”
10.Bendera ya Hispania Hispania
10.Bendera ya Misri Misri
09.Bendera ya Ujerumani Ujerumani
08.Bendera ya Uhindi India’HINDUS”
07.Bendera ya Brazil Brazil
06.Bendera ya Indonesia Indonesia
05.Bendera ya Japani Japan
04.Bendera ya South Korea Korea Kusini
03. Uturuki’OT3!”
02.Bendera ya Afrika Kusini Afrika Kusini
01. Ufalme wa Muungano
.:%#^.Bendera ya Uajemi Iran’P3RSIA’.:
Official language
FOUR-FIV3TE3N*LANGUAG3S’.:
G-20’+1/2”*: Chairman.:
Chairman; President ,etc.:
Main organ
UNITED NATIONS.;
Staff
351’Million +PR,China=1.453+ Billion.:
Volunteers
GROUP OF SEV3N & BRICS Group.:
Jedwali la nchi 20 tajiri zaidi duniani.

Kundi la Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu Ishirini (linalojulikana kama G-20, G20 au Group of Twenty) ni kundi la mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka nchi zenye uchumi mkubwa duniani: nchi 20, kuongezea Umoja wa Ulaya.

Kwa pamoja, uchumi wa G-20 unajumuisha 85% ya[2] bidhaa jumla zinazotoka katika nchi[2] ulimwenguni, 80% ya biashara duniani (pamoja na biashara ya EU ya ndani) na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani.[3]

G-20 ni kama ukumbi wa ushirikiano na kushauriana kuhusu masuala ya mfumo wa fedha wa kimataifa. Husoma, kupitia upya, na kukuza majadiliano kati ya nchi muhimu za viwanda na soko zinazoibukia kuhusu masuala ya sera zinazohusu uendelezaji wa udhibiti wa fedha kimataifa, na hutaka kushughulikia masuala ambayo yako juu ya majukumu ya shirika lolote.!!

Kwa G-20 kuongeza nguvu tangu kongamano la Washington la mwaka 2008, viongozi wake walitangaza tarehe 25 Septemba 2009, kwamba kundi hilo lingechukua pahala pa G8 kama halmashauri kuu ya kiuchumi ya mataifa tajiri.[4]

Viongozi wa mataifa wanachama wa G-20 hukutana kila mwaka mara mbili katika Kongamano la G-20.

Mpangilio

G-20 hufanya kazi bila sekretarieti ya kudumu wala wafanyakazi. Uenyekiti huzunguka kila mwaka kati ya wanachama na huchaguliwa kutoka kwa kambi tofauti za nchi. Mwenyekiti ni mmoja wa memba wa kundi la usimamizi la watatu la zamani, sasa na wenyekiti wa baadaye lifahamikalo kama Troika. Mwenyekiti wa sasa huunda sekretarieti ya muda kwa wakati wake, ambayo inaratibu kazi ya kikundi na kupanga mikutano yake. Jukumu la Troika ni kuhakikisha mwendelezo wa kazi za G-20 na usimamizi katika miaka ijayo. Ifuatayo ni orodha ya nchi wenyekiti wa G-20:[5]

Year Nchi Mwenyekiti
2001 Ujerumani
2001 Kanada
2002 Uhindi
2003 Meksiko
2004 Ujerumani
2005 Jamhuri ya Watu wa China
2006 Australia
2007 Ufaransa
2008 Marekani
2009 Uingereza
2010 Korea Kusini
2011 Ufaransa
2012 Meksiko
2013 Urusi
2014 Australia
2015 Uturuki
2016 Jamhuri ya Watu wa China
2017 Ujerumani
2018 Argentina
2019 Japani
2020 Saudia
2021 Italia
2022 Indonesia
2023 Uhindi

Mwanachama wa 20 ni Umoja wa Ulaya ambao unawakilishwa na Rais wa Baraza la Ulaya na Benki Kuu ya Ulaya

Kuongezea wanachama hawa 20, vikao na taasisi zifuatazo, zikiwakilishwa na maofisa watendaji wakuu, hushiriki katika mikutano ya G-20:

Uanachama

Uanachama wa G-20 unajumuisha:

Uanachama hauonyeshi kabisa nchi 19 zenye uchumi mkubwa duniani katika mwaka. Shirika hili linasema:[6]

kwa ukumbi kama wa G-20, ni muhimu hasa kwa nchi wanachama kuzuiuwa na kufuata kanuni kuhakikisha kuenda vyema na uendelevu kwa shughuli zake. Hakuna vigezo rasmi vya kujiunga na G-20 na mtungo wa kikundi hiki umekuwa haujabadilika tangu kilipoanzishwa. Kwa kuangalia malengo ya G-20, ilifikiriwa ni muhimu kuwa nchi na kanda zenye umuhimu kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa zijumuishwe. Mambo kama vile usawa wa Jiografia and kuwakilishwa kwa umma pia yalichangia pakubwa.

Mataifa yote wanachama 19 ni kati ya chumi bora 32 kama ilivyo pimwa katika Pato la Taifa kwa bei nomino katika orodha iliyochapishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mwaka 2008.[7] Nchi ambazo hazijawakilishwa katika G-20 ni Uswisi (19), Norway (25), Taiwan (26), Iran (28) na Venezuela (31), hata ingawa wako juu ya orodha kuliko baadhi ya wanachama. Uhispania (9), Uholanzi (16), Poland (18), Ubelgiji (20), Uswizi (22), Austria (24), Ugriki (27) na Denmark (29) wanawakilishwa tu kama memba wa EU, wala si memba kamili. Wakati Pato la Taifa linapimwa kwa viwango vya nguvu za ununuzi (PPP), wanachama wote 19 ni kati ya bora 24 duniani katika mwaka 2008, kulingana na IMF.[8] Iran (17), Taiwan (19) na Thailand (23) si wanachama wa G-20, huku Uhispania (12), Uholanzi (19) na Poland (20)wakijumuishwa tu katika kipengele cha EU. Hata hivyo, katika orodha ya wastani wa Pato la Taifa, iliyokadiriwa kwa miaka tangu kuundwa kwa kundi hili (1999-2008) kwa viwango vyote vya nomino na vya PPP, Uhispania, Uholanzi, Taiwan, na Poland tu ndiyo wanaonekana juu ya mwanachama yeyote wa G-20 katika orodha zote mbili mtawalia.[9]

Mara nyingi inasemekana kwamba G20, ingawa inatoa uwakilishi mpana zaidi kuliko G8, haina haki ya kufanya maamuzi yanayoathiri dunia nzima, kwa sababu wanachama wake wanachaguliwa bila kanuni zozote. G20 haina mkataba na mijadala yake si ya faraghani, hivyo kuifanya "taasisi isiyo yakidemokrasia." [10] Wakosoaji wanapendekeza mbadala kama vile Baraza la Usalama wa Kiuchumi katika Umoja wa Mataifa, ambapo wajumbe wanapaswa kuchaguliwa na Mkutano Mkuu kufuatia umuhimu wao katika uchumi wa dunia na mchango walio tayari kutoa kwa maendeleo ya uchumi wa dunia.[11]

Historia

G-20 Leaders Summit on Financial Markets na Uchumi Duniani mjini Washington, D.C. tarehe Novemba 2008

G-20, ambayo ilichukua pahala pa G-33, ambayo pia ilikuwa imechukua pahala pa G22, ilitajwa katika mkutano wa G7 mjini Cologne mnamo Juni 1999, lakini ilianzishwa rasmi katika Mkutano wa G7 wa mawaziri wa fedha mnamo tarehe 26 Septemba 1999. Mkutano wa uzinduzi ulifanyika mnamo tarehe 15-16 Desemba 1999 mjini Berlin. Mwakani 2008 Uhispania na Uholanzi waliongezwa kwa mwaliko wa Ufaransa katika Mkutano wa G-20 wa Viongozi kuhusu masoko ya fedha na Uchumi Duniani.

Mnamo 2006, kaulimbiu ya mkutano wa G-20 ilikuwa "Kujenga na Kuendeleza mafanikio. Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na mageuzi ya ndani ili kufikia "ukuaji endelevu", nishati ulimwenguni na masoko ya rasilimali, 'marekebisho' ya Benki ya Dunia na IMF, na athari za mabadiliko demografiki kutokana na idadi ya wanaozeeka. Trevor A. Manuel, Mbunge, Waziri wa Fedha, Afrika ya Kusini, alikuwa mwenyekiti wa G-20 wakati wa Afrika ya Kusini ilikuwa mwenyeji wa Sekretarieti ya mwaka 2007. Guido Mantega, Waziri wa Fedha, Brazili, alikuwa mwenyekiti wa G-20 mwaka 2008; Brazili ilipendekeza mazungumzo juu ya ushindani katika masoko ya fedha, nishati safi na maendeleo ya kiuchumi na vipengele vya fedha vya ukuaji na maendeleo. Katika taarifa kufuatia mkutano wa G7 mawaziri wa fedha tarehe 11 Oktoba 2008, Rais wa Marekani George W. Bush alisema kuwa mkutano ujao wa G-20 utakuwa muhimu katika kutafuta jawabu la (uliyoitwa kwa wakati huo) mgogoro wa kiuchumi wa 2008. Mpango wa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown ulipelekea kuweko kwa mkutano maalum wa G-20, Kongamano la Viongozi wa G-20 kuhusu masoko ya fedha na uchumi wa dunia, mnamo tarehe 15 Novemba 2008.[12] Viongozi wa G20 walikutana tena mjini London mnamo tarehe 2 Aprili 2009.[13] Kongamano lingine la G20 yalifanyika mnamo 24-25 Septemba 2009 mjini Pittsburgh, Pennsylvania. [14]

Mikutano ya G-20

Kongamano la G-20 lilianzishwa kama itikio kwa tatizo wa kifedha la 2007-2010 na pia kwa kuonekana kwamba nchi zinazostawi hazikuwa zimejumuishwa vya kutosha katika majadiliano ya kiuchumi duniani na utawala. Makongamano ya G-20 ya wakuu wa nchi au serikali yalifanyika mbali na Mikutano ya G-20 ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu ambao waliendelea kukutana kuandaa Kongamano la wakuu wa nchi na pia kutekeleza maamuzi yao.

Tarehe Nchi mwenyeji Jeshi mji
1 [15] Novemba 2008  Marekani Washington, DC, USA
2 [15] Aprili 2009  Ufalme wa Muungano London, England, UK
3 [15] Septemba 2009  Marekani Pittsburgh
4 [16] Juni 2010  Kanada Toronto
5 [17] Novemba 2010  South Korea Busan
6 [18] 2011  Ufaransa Toulouse

Mikutano ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu:

Mmenyuko wa Umma

Tangu mwaka 1999, G-20 mikutano mingi ya G-20 imekuwa ikipingwa. Maandamano mengi huanza kwa amani, lakini mingi hugeuka vurugu na watu wengi hujeruhiwa na uharibifu wa mali katika maeneo ya mitaa. Sababu hasa za maandamano hubadilika kutoka mkutano hadi mwingine, na hata maandamano mengi wakati wa mkutano mmoja. Hata hivyo, hisia tele na kuguna kwa waandamanaji hakujabadilika. Kama ilivyodhahiri,ukweli ni kwamba maandamano hayo yamekuwa yakiendelea tangu mwaka 1999, na yamendelea kuisha kwa vurugu. Habari zaidi kuhusu maandamano ya mikutano hasa inaweza kupatikana kwenye kurasa za mikutano hiyo katika sehemu ya Angalia Pia.:

Maeneo ya dunia kwa utajiri (idadi ya dola trilioni).

Angalia Pia

.:

Maelezo

  1. FAQ #5: What are the criteria for G-20 membership? Archived 6 Mei 2013 at the Wayback Machine. from the official G-20 website
  2. 2.0 2.1 "No Clear Accord on Stimulus by Top 20 Industrial Nations." The New York Times, ukurasa A1, 15 Machi 2009.
  3. Uanachama wa G-20 Archived 4 Mei 2011 at the Wayback Machine. kutoka tovuti rasmi ya G-20
  4. "Officials: G-20 to supplant G-8 as international economic council", CNN, 2009-09-25. Retrieved on 2009-09-25. 
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-04. Iliwekwa mnamo 2010-01-21. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  6. FAQ # 5: Je, nini vigezo vya uanachama wa G-20? Archived 6 Mei 2013 at the Wayback Machine. kutoka tovuti rasmi ya G-20
  7. World Economic Outlook Database-Oktober 2008, Shirika la Fedha la Kimataifa.
  8. World Economic Outlook Database, Aprili 2009, Shirika la Fedha la Kimataifa
  9. GDP (Nominal). GDP (PPP) World Economic Outlook Database, Aprili 2009, Shirika la Fedha la Kimataifa
  10. G20 yapaswa kuongezwa hadi Bilioni 6 Archived 21 Januari 2010 at the Wayback Machine. Daniele Archibugi, Opendemocracy.net
  11. Baraza la uchumi na Usalama wa Jamii la Umoja wa Mataifa Frances Stewart na Sam Daws, Oxford University, Machi 2001
  12. Kongamano la G-20: je, linahusu nini?, Kutoka Taasisi ya Brookings
  13. Uingereza kuwa wenyeji wa mkutano G-20 wa kifedha "Novemba Archived 2008-12-09 at the UK Government Web Archive 26, 2008 kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza
  14. Marekani kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 unaofuata BBC News, 28 Mei 2009
  15. 15.0 15.1 15.2 Kongamano la viongozi wa G-20 kuhusu Masoko ya hisa na Uchumi Duniani Archived 9 Novemba 2016 at the Wayback Machine. kutoka senta ya habari za G-20 I katika Chuo Kikuu cha Toronto
  16. Kanada kuwa mwenyeji wa kongamano 'mpito' la mwaka 2010
  17. "Korea to Host G20 in November", The Korea Times, 25 Septemba 2009. Retrieved on 26 Septemba 2009. 
  18. Pointi ya 31 kutoka tamko la viongozi katika kongamano la Pittsburgh 2009 Archived 14 Mei 2011 at the Wayback Machine.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: