Nenda kwa yaliyomo

Ngome

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngome ya Yesu mjini Mombasa ni mfano mashuhuri wa ngome katika Afrika ya Mashariki.

Ngome (kwa Kiingereza castle, fort) ni jengo kubwa lililoimarishwa kwa shabaha ya kujihami dhidi ya maadui na kujitetea dhidi ya mashambulio.

Kutokana na maendeleo ya teknolojia ya silaha za moto ngome hazitumiwi tena kwa kusudi hizi. Lakini ngome nyingi duniani zimebaki kama ushuhuda wa kihistoria wa karne zilizopita. Ilhali ngome zilijengwa kwa kuta nene na muundo imara, mabaki yao yamedumu miaka mingi.