Nenda kwa yaliyomo

Ottawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ottawa, Kanada






Ottawa

Bendera
Ottawa is located in Kanada
Ottawa
Ottawa

Mahali pa Ottawa katika Kanada

Majiranukta: 45°25′15″N 75°41′24″W / 45.42083°N 75.69000°W / 45.42083; -75.69000
Nchi Kanada
Mkoa Ontario
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 812,129
Tovuti:  http://www.ottawa.ca/
Barabara ya Elgin mjini Ottawa
Majengo ya Bunge la Kanada

Ottawa ni mji mkuu wa Kanada ikiwa ndani ya eneo la jimbo la Ontario. Mji uko kusini ya mto Ottawa. Mwaka 2004 ilikuwa na wakazi 800,000 mjini, pamoja na mitaa ya jirani rundiko la mji lina wakazi 1,146,790.

Ottawa ni mji mkubwa wa nne katika Kanada. Wakazi walio wengi hutumia Kiingereza lakini takriban theluji moja ni wasemaji wa Kifaransa kama lugha ya kwanza.

Mto Ottawa wakati wa usiku

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ottawa iliundwa 1827 ikaitwa mwanzoni Bytown kufuatana na kanali John By aliyesimamia ujenzi wa mfereji kati ya mto Ottawa na mto Rideau na kuanzisha mji vilevile.

Tangu 1857 mji uliteuliwa kama mji mkuu wa koloni ya Amerika ya Kaskazini ya Kiingereza na kuitwa kwa jina la mto Ottawa.

Mahali paliteuliwa kwa sababu ya hofu za vita mpya na Marekani; miji mingine mikubwa ilikuwa karibu mno na mpaka wa Marekani. Faida nyingine ya Ottawa ilikuwa mahali pake kwenye mstari wa mpaka wa ndani kati ya maeneo yanayotumia zaidi lugha ya Kiingereza au lugha ya Kifaransa. Kwa namna hii ilikubaliwa na Wakanada wa kundi zote mbili.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ottawa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.