Nenda kwa yaliyomo

Theodoro wa Studion

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Theodoro wa Studion katika mozaiki ya karne ya 11, Chios.

Theodoro wa Studion (Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 759[1] – Cape Akritas, Bitinia, 826) alikuwa mmonaki, halafu abati wa monasteri ya Studion mjini.[2]

Aliifanya kuwa shule ya wasomi, watakatifu na wafiadini wahanga wa dhuluma za waliopinga heshima kwa picha takatifu. Kwa kutetea kwa nguvu heshima hiyo, bila kujali kwamba msimamo wake ulimvutia dhuluma kutoka kwa kaisari na patriarki zilizoathiri sana afya yake, alipelekwa uhamishoni mara tatu.

Pia alishika nafasi muhimu katika kufufua umonaki na fasihi huko Bizanti.

Akiheshimu sana mapokeo ya Mababu wa Kanisa na ili kufafanua imani sahihi aliandika vitabu maarufu kuhusu mada za msingi wa mafundisho ya Kikristo.

Kati ya vitabu vyake vingi, barua kuhusu urekebisho wa monasteri ndiyo maandishi ya kwanza kupinga utumwa.[3][4]

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[5] au 12 Novemba.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Chisholm 1911, "Theodorus—Theodosia", p. 769.
  2. Browne 1933, p. 76; Chisholm 1911, "Theodorus—Theodosia", p. 769.
  3. Halsall, Paul (Machi 1996). "Medieval Sourcebook: Theodore of Studium: Reform Rules". Fordham University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-14. Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Page 1929, p. 63.
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.