Will Smith
Will Smith | |
---|---|
Will Smith mnamo 2019 | |
Amezaliwa | Willard Christopher Smith, Jr. 25 Septemba 1968 Wynnefield, Philadelphia, Pennsylvania, West Philadelphia, Pennsylvania, U.S. |
Kazi yake | Mwigizaji, rapa, mtayarishaji wa filamu, mtayarishaji wa rekodi, mtayarishaji wa televisheni |
Miaka ya kazi | 1987–hadi leo |
Ndoa | Sheree Zampino (1992–1995) Jada Pinkett Smith (1997–hadi leo) |
Tovuti rasmi |
Willard Christopher "Will" Smith, Jr. (amezaliwa tar. 25 Septemba 1968)[1] ni mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, na rapa kutoka nchini Marekani. Amefurahia sana mafanikio yake ya kimuziki, televisheni na filamu. Gazeti la "Newsweek" limemwita mwigizaji mwenye uwezo mkubwa kabisa duniani.[2] Smith amewahi kushindanishwa kwenye tuzo za Golden Globe mara nne, Academy Awards mara mbili, na ameshinda matuzo kede-kede ya Grammys.
Smith ameanza kujibebea umaarufu akiwa kama rapa chini ya jina la The Fresh Prince mwishoni mwa miaka ua 1980 na jina la uhusika kwenye mfululizo wa televisheni wa The Fresh Prince of Bel-Air. Filamu maarufu ambazo kacheza ni pamoja na Bad Boys na mfululizo wake wa pili Bad Boys II; Men in Black na mfululizo wake wa pili Men in Black II; Independence Day; I, Robot ; Ali; The Pursuit of Happyness; I Am Legend; Hancock; na Seven Pounds. Yeye ni mwigizaji pekee katika historia kuwa na mfululizo wa filamu nane zilizopata mauzo ya dola za Kimarekani milioni 100 kwenye sanduku la ofisi la nyumbani na vilevile kuwa kama mwigizaji pekee kuwa na filamu nane mfululizo kushika nafasi ya kwanza kwenye siku ya uzinduzi wa nyumbani akiwa kama mwigizaji kiongozi.[3]
Familia na maisha ya mwanzoni
[hariri | hariri chanzo]Smith, ni Mwafrika-Mwamerika aliyezaliwa na kukulia mjini West Philadelphia na Germantown huko Northwest Philadelphia. Mama yake, Caroline, alikuwa msimamizi wa shule ambaye alifanya kazi kama msimamizi wa bodi ya shule Philadelphia, na baba yake, Willard Christopher Smith, Sr., alikuwa mhandisi wa majokofu.[4][5] Kiimani, alilelewa Kibaptist.[6] Wazazi wake walitengana akiwa na umri wa miaka kumi na tatu na kuja kupeana talaka rasmi akiwa na umri wa miaka thelathini na mbili.[7] Ucheshi wa Smiths na jinsi anavyoonekana akiwa shuleni, wakampa jina la utani kama "Prince", ambalo hatumaye likaja kugeuka na kuwa "Fresh Prince". Wakati yuujanani mwake, Smith akaanza kurao na hatimaye akaanza kushirikiana na Jeff Townes (a.k.a. DJ Jazzy Jeff), ambaye alikutana naye kwenye sherehe moja hivi. Akanza kuhudhuria kwenye shule ya Overbrook High School ya mjini West Philadelphia. DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince ilizaliwa na Smith huku yeye akiimba mistari wakati Townes anashughurikia suala zima la kusugua na kuchanganya midundo—mwungano huo ulikuwa gumzo sana kwenye nyanja za muziki wa hip hop hasa katika miaka ya 1980 na mwazoni mwa 1990.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- Big Willie Style (1997)
- Willennium (1999)
- Born to Reign (2002)
- Lost and Found (2005)
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Filamu | Uhusika | Mshahara (US$)[8] | Maelezo |
---|---|---|---|---|
1990 | Saturday Morning Videos | Host | TV | |
ABC Afterschool Special - "The Perfect Date" | Hawker | TV | ||
The Fresh Prince of Bel-Air | William "Will" Smith | TV (1990-1996) | ||
1992 | Blossom | Fresh Prince | TV, Kauza sura | |
Where the Day Takes You | Manny | 50,000 | ||
1993 | Made in America | Tea Cake Walters | 100,000 | |
Six Degrees of Separation | Paul | 500,000 | ||
1995 | Bad Boys | Detective Mike Lowrey | 2,000,000 | |
1996 | Independence Day | Captain Steven "Steve" Hiller, USMC | 5,000,000 | |
1997 | Men in Black | James Darrell Edwards / Agent J | 5,000,000 | |
1998 | Enemy of the State | Robert Clayton Dean | 14,000,000 | Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture |
1999 | Torrance Rises | Kauza sura | ||
Wild Wild West | Captain James "Jim" West | 7,000,000 | ||
2000 | Welcome to Hollywood | Yeye mwenyewe | ||
The Legend of Bagger Vance | Bagger Vance | 10,000,000 | Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture | |
2001 | Ali | Muhammad Ali | 20,000,000 | Kashindanishwa — Academy Award for Best Actor Kashindanishwa — Broadcast Film Critics Association Award for Best Actor Kashindanishwa — Golden Globe Award for Best Actor – Motion Picture Drama Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture |
2002 | Men in Black II | James Darrell Edwards / Agent J | 20,000,000 + 10% ya mapato ya filamu |
BET Award for Best Actor Kashindanishwa — Black Reel Awards of 2002 |
Girlfriend ya B2K | Yeyey mwenyewe | Muziki wa video | ||
2003 | Bad Boys II | Detective Mike Lowrey | 20,000,000 + 20% ya mapato yote ya filamu |
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture |
2004 | A Closer Walk | Mwadithiaji | Makala | |
Jersey Girl | Yeye mwenyewe | Kauza sura tu | ||
American Chopper | Yeye mwenyewe | TV, Kauza sura | ||
I, Robot | Detective Del Spooner | 28,000,000 | Mtayarishaji Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture | |
Shark Tale | Oscar | 15,000,000 | Sauti | |
2005 | There's a God on the Mic | Makala | ||
Hitch | Alex "Hitch" Hitchens | 20,000,000 | BET Award for Best Actor Kashindanishwa — Black Movie Award for Best Actor Kashindanishwa — Black Reel Awards of 2006 Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture | |
2006 | The Pursuit of Happyness | Chris Gardner | 10,000,000 + 20% of the gross |
Mtayarishaji
Kashindanishwa— Academy Award for Best Actor |
2007 | I Am Legend | Dr. Robert Neville | 25,000,000 | Mtayarishaji, Kashindanishwa — BET Award for Best Actor Kashindenishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture |
2008 | Hancock | John Hancock | 20,000,000 + 20% ya mapato ya filamu |
Mtayarishaji |
Lakeview Terrace | Mtayarishaji | |||
The Secret Life of Bees | Mtayarishaji | |||
Seven Pounds | Tim Thomas | Mtayarishaji | ||
2009 | The Mark[9] | |||
Unbroke: What You Need to Know About Money | Television special | |||
2010 | Time Share[10] | |||
2011 | I Am Legend: Awakening[11][12] | Robert Neville | ||
2012 | Men in Black III[13] | James Darrell Edwards / Agent J |
Soma zaidi
[hariri | hariri chanzo]- Doeden, Matt (2007). Will Smith. Minneapolis, Minnesota, United States: Lerner Publications, ISBN 0-8225-6608-7
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Jason Ankeny (2008). "Will Smith on MSN". MSN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-01-11. Iliwekwa mnamo 2008-07-17.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help) - ↑ Sean Smith. "The $4 Billion Man", Newsweek, 2007-04-09. Retrieved on 14 Februari 2009. Archived from the original on 2010-01-06.
- ↑ "WEEKEND ESTIMATES: 'Hancock' Delivers $107M 5-Day Opening, Giving Will Smith a Record Eighth Consecutive $100M Grossing Movie!; 'WALL-E' with $33M 3-Day; 'Wanted' Down 60 Percent for $20.6M; 'Kit Kittredge' a Disaster!". Fantasy Moguls. 2008-07-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-06. Iliwekwa mnamo 2008-07-07.
- ↑ Will Smith Biography (1968-)
- ↑ "Where there's a Will, there's a way", Taipei Times, 2004-08-09.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-19. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
- ↑ Rebecca Winters Keegan. "The Legend of Will Smith", Time, 2007-11-29. Retrieved on 2009-10-21. Archived from the original on 2007-12-01.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-06. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
- ↑ http://www.boxofficeprophets.com/tickermaster/listing.cfm?tmID=1216
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-29. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-27. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-22. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
- ↑ Brendon Connelly (21 Aprili 2010). "Barry Sonnenfeld Confirms Will Smith and Tommy Lee Jones For Men in Black 3D". /Film. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-19. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2010.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Official site
- Will Smith at the Internet Movie Database
- Will Smith katika Yahoo! Movies
- Will Smith katika People.com
- Will Smith discography katika MusicBrainz
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Will Smith kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |