Nenda kwa yaliyomo

Yuda Iskarioti : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: sh:Juda Iskariotski
Mstari 49: Mstari 49:
[[hr:Juda Iškariotski]]
[[hr:Juda Iškariotski]]
[[hu:Iskarióti Júdás]]
[[hu:Iskarióti Júdás]]
[[hy:Հուդա Իսկարիովտացի]]
[[id:Yudas Iskariot]]
[[id:Yudas Iskariot]]
[[ilo:Judas Iscariote]]
[[ilo:Judas Iscariote]]

Pitio la 17:53, 21 Oktoba 2010

Busu la Yuda lilivyochorwa na Beato Angelico

Yuda Iskarioti (kwa Kiebrania יהודה איש־קריות), alikuwa mmojawapo wa Mitume wa Yesu, maarufu kwa kuwa alimsaliti mwalimu wake apate vipande thelathini vya fedha (Injili ya Mathayo 26:14-16).

Ni tofauti na mtume mwenzake Yuda Tadei.

Mitume wa Yesu

Majina

Kwa Kigiriki, katika Agano Jipya anaitwa Ιουδας Ισκαριωθ (Ioudas Iskariôth) na Ισκαριωτης (Iskariôtês).

Kwa kuwa Yuda ni jina la babu wa kabila kubwa la Israeli lililobaki baada ya yale ya Kaskazini kupotea uhamishoni (722 K.K.), lilitumiwa sana na Wayahudi, hata wawili kati ya mitume hao wanaitwa hivyo. Ndiyo sababu ilibidi kuwatofautisha kwa jina la pili, ambalo kwake ni "Iskarioti", maana yake "mtu wa Kariot" (Ish Kariot) kutokana na kijiji cha asili (Keriot-Chezron kinachotajwa tu katika Kitabu cha Yoshua 15:25, kikiwa Kusini kwa Yudea, mipakani kwa Edomu, kwenye Neghev.

Tafsiri nyingine inategemea jina Ekariot ("gaidi") walilopewa wapiganajiuhuru wakali zaidi, waliokuwa tayari kuua wakoloni popote pale.

Tafsiri ya tatu inazingatia neno la Kiaramu sheqarya' au shiqrai, linalomaanisha mtu dhalimu; "tapeli" linaweza kutafsriwa ishqaraya.

Tafsiri ya mwisho inategemea neno lingine la lugha hiyo, sakar, yaani anayekabidhi.

Katika Agano Jipya

Yuda anatajwa katika Injili na mwanzoni mwa Matendo ya Mitume. Humo tunasoma kwamba alikuwa mtunzahazina wa kundi la Mitume (Injili ya Yohane 12:6) mwenye tabia ya udokozi ambaye hatimaye alimuuza Yesu kwa maadui wake wa Baraza la Israeli (Injili ya Mathayo 26:47-49). Mapema baada ya tukio hilo alikufa vibaya (30 B.K.) na nafasi yake ikashikwa na Mtume Mathia.

Viungo vya nje