Yakobo Mkubwa
Mitume wa Yesu |
---|
|
Yakobo, mwana wa Zebedayo na Salome, na kaka wa Mtume Yohane, alikuwa Myahudi wa karne ya 1 aliyepata kuwa mmoja kati ya Mitume wa Yesu walio muhimu zaidi[1].
Anaitwa "Mkubwa" ili kumtofautisha na Mtume mwingine mwenye jina hilohilo, Yakobo Mdogo mwana wa Alfayo.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Yakobo pamoja na baba na mdogo wake walikuwa wavuvi huko Kafarnaumu kwenye Ziwa Galilaya.
Wataalamu kadhaa wanadhani walikuwa pia makuhani.
Wito wa utume
[hariri | hariri chanzo]Inakadiriwa alikutana na Yesu mwaka 28.
Pamoja na mdogo wake waliitwa na Yesu Boanerghes ("wanangurumo") kutokana na umotomoto wao kitabia.
Pamoja na mitume wengine waliongozana na Yesu Kristo miaka mitatu hivi, ambapo Yakobo alionekana kuwa karibu sana na Yesu na kuchaguliwa naye kushuhudia matukio kadhaa ya pekee (ufufuo wa binti Yairo, kugeuka sura mlimani, kihoro bustanini).
Baada ya ufufuko wa Yesu
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kifo na ufufuko wa Yesu, Yakobo alishika nafasi ya maana katika jumuia ya kwanza ya Wakristo wa Yerusalemu.
Mwaka 44 hivi aliuawa na mfalme Herode Agripa I kwa upanga (Matendo ya Mitume 12:1-2), wa kwanza kumfia Yesu kati ya Mitume wake.
Heshima yake
[hariri | hariri chanzo]Anaheshimiwa na Wakristo wote kama mtakatifu, hasa tarehe 25 Julai[2] huko Santiago de Compostela (Hispania, ambapo wengine wanaamini aliwahi kufika kwa umisionari).
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "St. James the Great, Apostle", Butler's Lives of the Saints
- The Life, Miracles and Martyrdom of St. James the Great: Apostle and Martyr of the Christian Church Ilihifadhiwa 9 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine.
- The Way of St. James Guide for the pilgrimage to Santiago de Compostela following St. James's footsteps.
- Catholic Encyclopedia: St James the Greater
- R. A. Fletcher, Saint James's Catapult: The Life and Times of Diego Gelmírez of Santiago de Compostela Oxford University Press, 1984: chapter 3, "The Early History of the Cult of St. James"
- Apostle James the Brother of St John the Theologian Orthodox icon and synaxarion
- History
- St. James the Greater, Apostle at the Christian Iconography web site
- St. James the Greater from Caxton's translation of the Golden Legend
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yakobo Mkubwa kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |