Adolf Mkenda
Mandhari
Adolf Faustine Mkenda (alizaliwa Rombo, Kilimanjaro, mwaka 1963), ni Waziri wa Elimu wa Tanzania. Profesa mshirika wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwanasiasa ambaye kwa sasa ni mbunge wa Chama Cha Mapinduzi wa jimbo la Rombo tangu Novemba 2020.
Kazi ya kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania wa 2020, Mkenda aliteuliwa kama Waziri wa Kilimo katika Baraza la Mawaziri la 5 la Tanzania na Baraza la Mawaziri la 6 la Tanzania. Kabla ya uteuzi huu alihudumu katika nyadhifa tofauti kama Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii (2019-2020), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (2018-2019)[1] na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (2017-2018).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Adolf Mkenda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |