Nenda kwa yaliyomo

Endometriosisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Endometriosisi
Endometriosisi
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuGynaecology Edit this on Wikidata
ICD-10N80.
ICD-9617.0
OMIM131200
DiseasesDB4269
MedlinePlus000915
eMedicinemed/3419 ped/677 emerg/165
MeSHD004715

Endometriosisi ni ugonjwa ambapo tishu ambazo kwa kawaida hukua ndani ya uterasi hukua nje ya uterasi.[1] Dalili zake kuu ni maumivu ya pelvisi na utasa. Takribani nusu ya watu huwa na maumivu sugu ya pelvisi ilhali asilimia 70 ya maumivu hutokea wakati wa hedhi. maumivu wakati wa kushiriki ngono ni ya kawaida. Utasa hutokea kwa hadi nusu ya watu.[2] Endometriosisi inaweza kusababisha athari za kijamii na kiafya.[3] Dalili zisizo za kawaida sana hujumuisha zile za mkojo na utumbo. Takribani asilimia 25 ya wanawake hawawi na dalili.[2]

Kisababishi na utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Kisababishi hakiko bayana kikamilifu.[2] Masuala hatari hujumuisha kuwa na historia ya kifamilia ya hali hii. Mara nyingi ovari, neli za fallopio, na tishu zilizo karibu na uterasi huathirika; hata hivyo, katika visa vichache sana pia inaweza kutokea katika sehemu nyingine za mwili.[4] Maeneo ya endometriosisi huvuja damu kila mwezi jambo ambalo husababisha inflamesheni na kovu.[2][4] Uvimbe unaosababishwa na endometriosisi sio saratani. Kwa kawaida utambuzi huzingatia misingi ya dalili ikijumuishwa na upigaji picha wa kimatibabu. Biopsi ndio njia hakika zaidi ya utambuzi.[4] Visababishi vingine vya dalili sawa hujumuisha: sindromu ya choo inayowasha, sistitisi ya mwanya, na fibromiajia.[2]

Uzuiaji na matibabu

[hariri | hariri chanzo]

Dhibitisho la kujaribia hupendekeza kuwa matumizi ya mchanganyiko wa kontraseptivu za kunywa hupunguza hatari ya endometriosisi.[5] Mazoezi na kujiepusha na kiwango cha juu cha pombe pia kunaweza kuzuia.[4] Hakuna tiba ya endometriosisi, lakini matibabu kadhaa yanaweza kuboresha dalili.[2] Haya yanaweza kujumuisha dawa za maumivu, matibabu ya homoni au upasuaji. Dawa za maumivu zinazopendekezwa kwa kawaida huwa NSAID kama vile naproxen. Kunywa sehemu ya tembe za kudhibiti uzazi kwa kuendeleza aukifaa cha kuzuia mimba kilicho na projestojeni pia kunaweza kusaidia. Gonadotropini-inayotoa homoni agonisti inaweza kuongeza uwezo wa walio tasa kushika mimba. Utoaji wa endometriosisi kwa njia ya upasuaji unaweza kufanyika kwa wale ambao dalili hazidhibitiki kwa matibabu ya dawa.[4]

Epidemolojia

[hariri | hariri chanzo]

Endometriosisi imekadiriwa kutokea kwa takribani asilimia 6–10 ya wanawake.[2] Huwa ya kawaida sana kwa walio katika miaka yao ya thelathini na arobaini. [4] Husababisha vifo vichache hivi vikikadiriwa kuwa 200 ulimwenguni katika mwaka wa 2013.[6] Endometriosisi ilitambuliwa kuwa hali tofauti katika miaka ya 1920. Kabla ya wakati huo endometriosisi na adenomiosisi zilitambuliwa kuwa kitu kimoja. Haijabainika aliyekuwa wa kwanza kutoa maelezo ya ugonjwa huu.[7]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Endometriosis: Overview". http://www.nichd.nih.gov. 06/24/2013. Iliwekwa mnamo 4 March 2015. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help); External link in |website= (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 Bulletti C, Coccia ME, Battistoni S, Borini A (Agosti 2010). "Endometriosis and infertility". J. Assist. Reprod. Genet. 27 (8): 441–7. doi:10.1007/s10815-010-9436-1. PMC 2941592. PMID 20574791.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. Culley L, Law C, Hudson N, Denny E, Mitchell H, Baumgarten M, Raine-Fenning N (2013). "The social and psychological impact of endometriosis on women's lives: A critical narrative review". Human Reproduction Update. 19 (6): 625–639. doi:10.1093/humupd/dmt027. PMID 23884896.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 "Endometriosis". http://www.womenshealth.gov/. Desemba 5, 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-03. Iliwekwa mnamo 4 Machi 2015. {{cite web}}: External link in |website= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Vercellini P, Eskenazi B, Consonni D, Somigliana E, Parazzini F, Abbiati A, Fedele L (2011). "Oral contraceptives and risk of endometriosis: a systematic review and meta-analysis". Hum. Reprod. Update. 17 (2): 159–70. doi:10.1093/humupd/dmq042. PMID 20833638.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  6. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 Desemba 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMID 25530442. {{cite journal}}: |first1= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  7. Brosens, Ivo (2012). Endometriosis: Science and Practice. John Wiley & Sons. uk. 3. ISBN 9781444398496.