Harold Kroto
Mandhari
Sir Harold (Harry) Walter Kroto (amezaliwa 7 Oktoba 1939) ni mwanakemia kutoka nchi ya Uingereza. Jina lake la kuzaliwa ni Harold Krotoschiner; wazazi wake walikimbia utawala wa WaNazi huko Ujerumani kwa vile asili yao ni Wayahudi wa Poland. Mwaka wa 1955 walifupisha jina lao la familia liwe Kroto.
Kroto hasa alichunguza sifa na mfumo wa kaboni. Mwaka wa 1996, pamoja na Robert Curl na Richard Smalley alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia. Mwaka uleule alipewa cheo cha "Sir" cha Uingereza.
Makala hii kuhusu mshindi wa Tuzo ya Nobel bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Harold Kroto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |