Jimbo Katoliki la Bukoba
Mandhari
Jimbo Katoliki la Bukoba (kwa Kilatini Dioecesis Bukobaënsis) ni mojawapo kati ya majimbo 35 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa linahusiana na Jimbo Kuu la Mwanza.
Askofu wake ni Jovitus F. Mwaijage.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 13 Desemba 1951: Kuanzishwa kwa Apostolic Vicariate of Lower Kagera
- 25 Machi 1953: Kupandishwa hadhi kuwa dayosisi kwa jina la Rutabo
- 21 Juni 1960: Kubadilishiwa jina liwe Bukoba, makao mkuu wa mkoa wa Kagera.
Uongozi
[hariri | hariri chanzo]- Maaskofu wa Bukoba
- Askofu Jovitus F. Mwaijage (27 Januari 2024)
- Askofu Desiderius M. Rwoma (15 Januari 2013 - 1 Oktoba 2022)
- Askofu Nestorius Timanywa (26 Novemba 1973 - 15 Januari 2013)
- Askofu Placidus Gervasius Nkalanga, sasa O.S.B. (6 Machi 1969 – 26 Novemba 1973)
- Kardinali Laurean Rugambwa (21 Juni 1960 – 19 Desemba 1968)
- Maaskofu wa Rutabo
- Vicar Apostolic wa Lower Kagera
- Kardinali Laurean Rugambwa (13 Desemba 1951 – 25 Machi 1953)
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Eneo ni la kilometa mraba 8,608, ambapo kati ya wakazi 1,042,400 (2020) Wakatoliki ni 609,725 (58.5%) katika parokia 39.
Hao wanahudumiwa na mapadri 143, ambao kati yao 140 ni wanajimbo na 3 ni watawa. Hivyo kila mmojawao kwa wastani anahudumia waamini 4,263.
Jimbo lina pia mabruda 6 na masista 581.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya jimbo
- Giga-Catholic Information
- Catholic Hierarchy
- Jimbo katika tovuti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Hati Ob divinitus Ilihifadhiwa 14 Julai 2014 kwenye Wayback Machine., AAS 44 (1952), uk. 397
- Hati Quemadmodum ad Nos, AAS 45 (1953), uk. 705
- Hati Eminentissimus, AAS 52 (1960), uk. 912
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Bukoba kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |