Kemgesi
Kijiji cha Kemgesi | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mara |
Wilaya | Serengeti |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 3,000 |
Tovuti: www.kemgesi.simplesite.com |
Kemgesi ni kijiji kilichopo Mkoa wa Mara, wilaya ya Serengeti, tarafa ya Ikorongo, kata ya Nyamatare, Tanzania.
Kijiji cha Kemgesi kilianzishwa mnamo miaka ya 1950 wakazi wengi wakiwa ni wafugaji, wawindaji na wakulima waliohamia kwa lengo la uwindaji, ufugaji na kilimo ila walivutiwa na upatikanaji wa maji pamoja na ardhi yenye rutuba.
Wakazi wa Kemgesi ni Wangoreme waliohamia kutoka vijiji mbalimbali vya jirani kama Butanga, Nyamitita, Gabande, Majimoto, Makondose, Ikorongo n.k.
Familia za kwanza kuhamia Kemgesi ni zile za Matiko, Koromba, Magambo, Masama Gebani, Masiko Nyangogo, Mgaya Nyarokweri, Ruge, Kisabo Makori, Nyigana Nyisaba, Msamba n.k.
Kijiji cha Kemgesi kimepakana na kijiji kidogo cha Ring'wani kwa upande wa Kaskazini, kijiji cha Maburi kwa upande wa magharibi, kijiji cha Nyamatare katika upande wa mashariki na upande wa Kusini kimepakana na kijiji cha Nyamatoke. Kijiji cha Kemgesi kina mitaa minne ambayo ni Kemgongo 'A', Kemgongo 'B', Inyentero na Makondose kikiwa jumla ya wakazi wapatao 3000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.[1]
Kijiji kipo chini ya kilima kizuri cha Nyarogati ambapo kuna Center kubwa na tambarare za mbuga maarufu kama Mwibara ambayo imekuwa ikitumiwa kama malisho ya mifugo na kivutio kikubwa kwa wageni. Wakazi wa kijiji cha Kemgesi ni wafugaji na wakulima wa mazao ya nafaka kama vile mahindi, mtama na ulezi.
Kijiji hiki kina huduma mbalimbali za kijamii ikiwamo shule mbili za msingi na vyanzo mbalimbali vya maji kama vile kisima cha asili Waibwe na mto mkubwa wa Nyagitamankwe.
Kimichezo kijiji cha Kemgesi ni wapenzi na washabiki sana wa mpira wa miguu na kuna upinzani mkubwa wa jadi kati ya timu za Kemgongo 'A' na Kemgongo 'B'. Vilevile wanapenda kucheza ngoma za asili kama vile Eghikohi, Obhusamba, Okwibhaka, n.k.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Repoti Kuu ya Hesabu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2012" (kwa Kiingereza). Serikali ya Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2003-12-28.
Kata za Wilaya ya Serengeti - Mkoa wa Mara - Tanzania | ||
---|---|---|
Busawe | Geitasamo | Ikoma | Issenye | Kebanchabancha | Kenyamonta | Kisaka | Kisangura | Kyambahi | Machochwe | Magange | Majimoto | Manchira | Matare | Mbalibali | Morotonga | Mosongo | Mugumu | Nagusi | Natta | Nyamatare | Nyambureti | Nyamoko | Nyansurura | Rigicha | Ring'wani | Rung'abure | Sedeco | Stendi Kuu | Uwanja wa Ndege |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kemgesi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |