Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Wangurimi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kata ya Nyamatare -Kemgesi,Kijiji Cha Kemgesi kilichopo kata ya Nyamatare wilaya ya Serengeti mkoa Wa Mara. Kilianzishwa mwaka 1973-1976 wakati wa harakati za uanzishwaji wa vijiji awali kilijulikana Kama Kijiji Cha Nyambureti huku Kemgesi kikiwa Kama tawi la kichama kwa chama Cha mapinduzi CCM lakini baada ya mwaka 1976 kikaanzishwa rasimi kuwa Kijiji mama Cha Kemgesi,.

Kinajishughulisha na kilimo ,ufugaji ,siasa pamoja na Biashara kwa kiasi kidogo mfano Uuzaji wa nafaka,nguo,maduka na inakadiliwa kuwa Kijiji Cha Kemgesi kina wakazi 6780 na kina vitongoji vinne ambavyo ni kama vifuatavyo; Kemgongo"A",Kemgongo"B",Inyentero,Makondese. Kemgesi Ina hekari 1020 eneo na inatambalale za nyika ambayo hufaa kwa ufugaji wa mbuzi ,Ng'ombe,kondoo,kuku, njiwa,Bata na upande wa kilimo ni mashuhuli wa kilimo Cha mtama mwekundu,mahindi, pamba,alizeti,ufuta,maboga,mumunya,viazi,kunde,ufuta,karanga,mbogamboga na kiasi kidogo Cha mpunga kulingana na eneo hilo lipo ukanda wa Savana ambao hausitawishi sana mpunga.

Siasa za Kemgesi Kijiji Cha Kemgesi ni Kijiji kinacho kabiliwa na ushindani mkubwa wa kisiasa kutoka vyama viwili ambavyo ni CCM na CHADEMA ambavyo huwa na mchuano mkubwa sana ambao nyakati za uchaguzi huwa na mgawanyiko wa watu kimatabaka na hubadilishana vijiti vya uongozi tangia mfumo wa vyama vingi ulinyo Anza 1992-1994 mwenyekiti wa Kijiji alikuwa anaitwa David Maganya ,1994-1999 Mwenyekiti wa Kijiji akiwa John Ondika ,1999-2004 Nestory Nyamhanga,2004-2008 Garinga Nyamasisi(madibwi),2008-2014 Alfaxadi Magocha ,2014-2019 Mwita King'orori(spika),2019-2024 Chacha (Rimura).

Madiwani kuanzia mfumo wa vyama vingi 1995-2005 David Maganya Masama (vipindi viwili mfululizo),2005-2010 Chacha Nyamhanga Nyasaga (kipindi 1),2010-2015 David Maganya Masama awamu ya (tatu),2015-2020 Chembo Manyanya Iroga (kipindi 1),2020--2025 Getera Mtongori.

Elimu Kijiji Cha Kemgesi tangu kilipo anzishwa kilikuwa kina shule ya Msingi 1 ambayo ilikuwa inaitwa Ring'wani S/M na baadae mwaka 1978 ilianza ujenzi mwingine wa shule ya Msingi ambayo ni Kemgongo S/M na ilipofika 1998 Kijiji kikaungan na Kijiji Cha Nyambureti, Kemgesi,Nyamatare wakajenga shule ya sekondari iliyoitwa Nyambureti lakini 2000 ilfunguliwa rasimi na makamu wa Raisi Dr Omari All Juma na kuanza kutumia hilo jina la ufunguzi wa hiyo shule.,hivyo Kemgesi Ina wakazi waliopata elimu wa kutosha. Afya Kijiji Cha Kemgesi kujenga zahanati yake 1979 kikiwa na wahudumu wa afya 2 na baadae 1993 kiliongezewa wa hudumu wa Afya 2 na kufanya idadi kufikia 4 na mwaka 2010 kikapandishwa Hadi na kuwa kituo Cha Afya na kuongezewa wafanyakazi 6 na kufunga idadi ya wafanyakazi 10 Hadi Sasa,ni kituo Cha Afya kinachotoa huduma ya mama na mtoto na huduma za magongwa ya kuambukiza na mlipuko.

History ya wangoreme

[hariri chanzo]

Wangore waliaza harakati zao za kuhama kutoka kusini mwa Afrika baada ya mashambulizi mbalimbali yakiwemo vita ya makabila kati Yao na wakosa (hosa),vita na wadudu hatari walio shambulia mifugo yao na wao wenyewe kuugua homa ya matende na magonjwa mengine yaliyotokana na mbung'o, ukame uliowakabili kwenye tambalale ya mbuga (nyika) ya kiluga ambayo Leo inajulikana Kama kluggel National park.

mnamo mwaka 1320 kutoka katika nyika ya kluggel na iliyo wapelekea kukimbia huku na kule Hadi kufika  kusini ya Tanganyika Leo ikijulikana (Tanzania) munamo mwaka 1748 walingilia ukanda wa nyasa kutafuta hifadhi ya seluhu Hadi kuifikia Mikumi kwani ni kabila ambalo walipenda kuishi na wanyama Kama walivyo Wamasai na baadae 1886 wakaingia bonde la Ngorongoro na wakaendelea kujishughulisha na kilimo na ufugaji Kama ilivyo jadi yao na hatimaye wakakutana  na kabila moja ambalo waliingiliana misamiati ya (kimatamshi,muundo,mtindo,maana),tamaduni na miiko.

Kabila hilo walijulikana Kama Wasonjo ambao walipatikana ukanda wa Loliondo pamoja na Wamasai waliokuwa wenyeji sana wa bonde la Ngorongoro na wahadizabe (karibu na ukanda wa mto wa mbuu) waliishi hapo na jamii hiyo ya wasonjo kwa furaha na upendo lakini Ilipofika mwaka 1919-1932 walianza kusumbuana na kabila la Wamasai kwa kunyang'anywa mifugo yao Kila itwapo Leo ikawalazimu kuanza kuhama ili wasiendelee kusumbuana na Wamasai kwa kufuata tambalale za mbuga ya Serengeti na ilipofika 1945 wakawa wamefika sehemu mbalimbali za Serengeti wakiwa ni wanzilishi wa Mji wa mugumu wakiongozwa na kiongozi wao aliyeitwa Sabayaya na mdogo wake aitwaye Koma ambaye yeye alikataria maeneo ya forti Ikoma hapo waliishi vizuri huku wakijishughulisha na kilimo,ufugaji,maeneo ya Mangwesi na walianza kuzaliana kwa kwa Kasi kubwa iliyo pelekea kutapakaa sehemu nyingi za Serengeti. 1970 vita Kali kati ya wangoreme na wakuriya ikapamba moto Maeneo ya Kibaso wakati wakuriya walipo iba Ng'ombe za mzee Mokena na inakadiliwa kuwa vita hiyo ilikuwa mbaya sana kwani takiribani watu 86 waliaga Dunia kwenye vita hivyo akiwemo Mgaya -Nyamori wa majimoto Mwita-Maro wa kisaka na wengineo wengi.

1989 vita ya pili kati ya wakuriya na wangoreme ikapamba moto Tena baada ya wakuriya kuiba Ng'ombe za mzee Mgaya(Nyarokweli) na Motondi waliokuwa wanaishi maeneo ya tambalale za nyika za Kemgesi inakadiliwa watu wapatao 34 walipoteza maisha.

Wangoreme Wanapatikana kwa wingi huko Iramba (Ngoreme), Majimoto, Busawe, Gantamome, Kisaka Nyiboko, Nyansurumunti, Gantamome, Busawe, Mesaga, Kenyamonta, Remung'oroli, Maburi, Gusuhi, Kemgesi, Masinki, Magange, Ring'wani, Kenyana, Nyamatoke, Mosongo, Nyamitita na Bolenga.

Lugha yao ni Kingurimiambayo waliweza kutambua miezi yote kumi na mbili kwa majina yao Kama vile mwezi 1-kyero kembele(January),2-Itaturi(February),3-Kimagha(March),4-Etwigho(April),5-Kyero ghekaphere(May),6-Kimagha ghekaphere (Juni),7-Nyamapheho(Julay),8-Ringura masaringi(Agost),9-Nyasahi(September),10-Kemwamu(October),11-Rughaka(November),12-Kemwamu kemwisho(Desember).

Ni wafugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo, mbwa kwa ulinzi wa mifugo, paka na punda: hiyo ndiyo asili yao.

Chakula cha asili ni ugali wa ulezi, mtama, mhogo, mahindi pia kunde, njugumawe, maboga, karanga.

Watani wa Wangurimi ni Wanyiramba na Wamasai Vilevile wangoreme wamepakana na kabila la wakuriya jamii ya wanyabasi,wakira ,wairenge,wakenye upande wa kaskazini-mashariki -Serengeti (Northeast-Serengeti).

Wangoreme ni wakarimu sana na wanapenda maendeleo, pia ni watu ambao wanapenda sana siasa. Kuna ushindani mkubwa, hasa kati ya vyama viwili: CCM na [[CHADEMA]. Na niwatu wanaopenda kufuata Mira na desturi za kingoreme mfano Jando na unyago kwa vijana waliofikia Rika la kuwa na majukumu ya kifamilia [Saro] Afya na elimu kwa wangoreme Wangoreme Wana shule mbalimbali Kama vile majimoto S/M iliyo jengwa 1951,Ngoreme S/S ilijengwa mwaka 1958,shule ya Msingi Ring'wani iliyo jengwa 1961. Masama Daud (majadiliano) 12:11, 12 Machi 2022 (UTC)[jibu]