Nenda kwa yaliyomo

Wete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wete
Wete is located in Tanzania
Wete
Wete

Mahali pa mji wa Wete katika Tanzania

Majiranukta: 5°3′36″S 39°42′36″E / 5.06000°S 39.71000°E / -5.06000; 39.71000
Nchi Tanzania
Mkoa Pemba Kaskazini
Wilaya Wete
Ramani ya Wete (Pemba)
Mahali pa Wete katika Pemba

Wete ni wilaya katika mkoa wa Kaskazini Pemba uliopo kaskazini mwa kisiwa cha Pemba yenye postikodi namba 75100 .

Ikiwa ina wakazi 107,916[1] kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, ni mji mkubwa kwa Pemba pia makao makuu ya Mkoa wa Pemba Kaskazini na pia ya Wilaya ya Wete.

Umbali na Chake Chake ni kilomita 20.

Bunge la Zanzibar lina jengo huko Wete linalotumiwa kwa ajili ya mikutano ya bunge kisiwani Pemba.

Bandari ya Wete ilikuwa muhimu lakini haifai kwa meli kubwa, tena haikutengenezwa ipasavyo baada ya kujengwa kwa bandari ya Mkoani. Lakini bado karafuu kutoka kaskazini ya Pemba zasafirishwa kupitia bandari ya Wete.

Kuna hospitali. Maghofu ya jumba la Mtambwe Mkuu yako kwenye kisiwa kidogo karibu na Wete.

Mauaji ya Wete 2001

[hariri | hariri chanzo]

Katika chaguzi za vyama vingi tangu mwaka 1995 wakazi wengi wa Wete, jinsi wakazi wa Pemba kwa jumla, walipendelea chama cha CUF. Kiongozi wa CUF Seif Shariff Hamad alikuwa mwenyeji wa Wete.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 wafuasi wa CUF waliona ya kwamba matokeo ya kura hayakuwa ya kweli na tarehe 27 Januari 2001 maelfu ya wananchi walikusanyika Wete kudai uchaguzi urudiwe.

Askari za Polisi walikuwa na amri kuzuia maandamano, hivyo yalivunjwa na polisi kwa ukali mkubwa. Waandamanaji angalau 13 waliuawa, 213 walijeruhiwa na zaidi ya 400 walikamatwa. Polisi pamoja iliendelea kutafuta wapinzani katika siku zilizofuata; kuna taarifa ya kwamba watu wengi walipigwa na wanawake kunajisiwa. Zaidi ya watu 2,000 kutoka Pemba walikimbilia Kenya kwa maboti madogo walipoishi katika makambi ya wakimbizi, hasa Shimoni.

  1. "Sensa ya mwaka 2012, Mkoa wa Pemba Kaskazini" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-03-29. Iliwekwa mnamo 2018-03-23.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]