Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili wa Shirika la Wikimedia
Sera hii imepitishwa na Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia. Lazima isiepwe, isivunje, wala isipuuzwe na viongozi au wafanyakazi wa Shirika la Wikimedia, wala sera za mradi wowote fulani wa Wikimedia. |
Sababu ya Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili
Mwongozo huu wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (UCoC) unatoa tafsiri ya tabia inayokubalika na isiyokubalika katika harakati za shirika la Wikimedia. Mwongozo huu utatumika kwa kila mmoja ambaye kwa namna moja ama nyingine anahusika na uchangiaji wa maudhui katika miradi ya Wikimedia Foundation mtandaoni , nje ya mtandao au katika sehemu yoyote ambapo shughuli za Wikimedia zinafanyika. Mwongozo huu utafuatwa na wanawikimedia wote yaani wachangiaji wapya na wazoefu, vyombo mbalimbali vya utendaji katika miradi ya Wikimedia Foundation, wafanyakazi na wajumbe wa bodi. Mwongozo huu pia utatumika katika mikutano yote yaani ya ana kwa na ile ya mtandaoni, sehemu mbalimbali ambazo miradi ya Wikimedia itakuwa ikifanyika, katika miradi yote ya Wikimedia pamoja na katika Wiki (Wikipedia) zote.
Tunataka jumuiya hizi kuwa na mawazo chanya, salama na mazingira wezeshi kwa yeyote anayejiunga nao. Pia, tunanuia kuilinda miradi yetu dhidi ya hao wanaoiharibu na kupotosha maudhui yaliyomo kwenye miradi yao.
Mwongozo wa UCoC utatumika kwa wanajumuiya wote bila ubaguzi wa aina yoyote. Kwenda kinyume na UCoC kunaweza kusababisha mtu husika kuwekewa vikwazo na wawakilishi na watendaji wa mradi husika (kulingana na mazingira ya kiutekelezaji wa jumuiya husika ) au shirika la Wikimedia Foundation lenyewe linaweza kuweka vikwazo hivyo likiwa kama mmiliki halali wa miradi yake.
- Private, public and semi-public interactions
- Discussions of disagreement and expression of solidarity across community members
- Issues of technical development
- Aspects of content contribution
- Cases of representing affiliates/communities with external partners
1 – Mwanzo
The Universal Code of Conduct provides a baseline of behaviour for collaboration on Wikimedia projects worldwide. Communities may add to this to develop policies that take account of local and cultural context, while maintaining the criteria listed here as a minimum standard.
The Universal Code of Conduct applies equally to all Wikimedians without any exceptions. Actions that contradict the Universal Code of Conduct can result in sanctions. These may be imposed by designated functionaries (as appropriate in their local context) and/or by the Wikimedia Foundation as the legal owner of the platforms.
2 – Mwenendo unaotarajiwa
Kila mwanawikimedia, bila kujali kama ni mchangiaji mgeni au mzoefu, mtendaji wa jumuiya, mshirika au mjumbe wa bodi wa WMF au mwajiriwa, atawajibika kwa tabia yake.
Katika miradi yote ya Wikimedia, maeneo mbalimbali na matukio, tabia itatakiwa kuwa kitu cha msingi kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na utu, ujamaa, mshikamano na uraia mwema. Dhana hii itatumika kwa wachangiaji na washiriki wote kuhusu namna wanavyohusiana na wachangiaji pamoja na washiriki wengine bila ubaguzi wa kujali umri, kuwa sawa au na ulemavu kiakili, mwonekano wa nje wa mwili wa mtu, utaifa, udini, ukabila, asili ya kitamaduni, tabaka, tabaka la kijamii, uwezo wa kuongea lugha kwa ufasaha, mwelekeo wa kijinsia, utambulisho wa kijinsia, au eneo la kazi ambalo mtu anafanyia kazi. Wala hatutatakiwa kumtofautisha mtu kwa kigezo cha mafanikio, ujuzi au msimamo wake katika miradi ya Wikimedia au harakati zake.
2.1 – Kuheshimiana
Heshima ni kuonyesha kujali wengine. Katika kuwasiliana na watu, iwe katika mazingira ya mtandaoni au nje ya mtandao wa Wikimedia, tutawaheshimu kwa heshima kama vile na sisi tungetaka watuheshimu.
Hii ni pamoja na (na vingine ambavyo havijatajwa hapa, lakini vinafanana na hivi vilivyoelezwa hapa chini ):
- Jitahidi kuwa mwelewa. Sikiliza na jaribu kuelewa kile ambacho Mwanawikimedia yeyote anataka kukuambia. Kuwa tayari kuibua changamoto na kubadilisha uelewa wako mwenyewe, matarajio na tabia yako kama Mwanawikimedia.
- Daima chukulia kitu kwa nia njema, na ushiriki katika uhariri mzuri wa kujenga, uhariri chanya. Toa na pokea maoni kwa upole na kwa nia njema. Ukosoaji unatakiwa ufanyike katika namna ya kujali, namna ya kujenga, na uhusishe mikakati halisi, yenye kupimika juu ya namna ya kuliboresha jambo unalolikosoa.
- Heshimu vile wachangiaji wanavyopenda kujiita na kujielezea wenyewe. Watu wanaweza kutumia maneno fulani kujielezea wenyewe. Kama ishara ya heshima, tumia maneno haya pale unapowasiliana nao au unapoelezea kitu kinachowahusu watu hawa. Mfano inaweza kuwa:
- Kundi fulani la kikabila linaweza kutumia jina fulani kujielezea lenyewe, badala ya jina la kihistoria linalotumiwa na watu wengine kuwaelezea watu hao.
- Watu wenye majina yanayotumia herufi za kipekee, sauti/matamshi, au maneno kutoka katika lugha zao, na alama hizo zinaweza kuwa hazijazoeleka kwako.
- People who identify with a certain sexual orientation or gender identity using distinct names or pronouns;
- People having a particular physical or mental disability may use particular terms to describe themselves
- During in-person meetings, we will be welcoming to everyone and we will be mindful and respectful of each other's preferences, boundaries, sensibilities, traditions and requirements.
2.2 - Utu, Ujamaa, mshikamano na uraia mwema
We strive towards the following behaviours:
- Civility is politeness in behaviour and speech amongst people, including strangers.
- Collegiality is the friendly support that people engaged in a common effort extend to each other.
- Mutual support and good citizenship means taking active responsibility for ensuring that the Wikimedia projects are productive, pleasant and safe spaces, and contribute to the Wikimedia mission.
Hii ni pamoja na(na vingine ambavyo havijatajwa hapa, lakini vinafanana na hivi vilivyoelezewa hapa chini)
- Ushauri na ufundishaji:' Kusaidia wageni kuelewa wanachotakiwa kufanya na kupata ujuzi muhimu.
- Onyesha mshikamano. Watafute wachangiaji wenzako, washike mkono pale wanapohitaji msaada, na wasemee pale wanapofanyiwa mambo ambayo yanakosa kiwango chetu.
- Tambua na sifu kazi iliyofanywa na wachangiaji: Washukuru kwa msaada ambao wamekupa. Thamini juhudi zao na toa sifa pale inapostahili.
3 – Mwenendo usiokubalika
Mwongozo wa kimataifa wa Mwenendo na Maadili unalenga kuwasaidia wanajamii kutambua aina au hali zinazopelekea tabia kuwa mbaya au ya kiunyanyasaji katika harakati za Wikimedia.Tabia zifuatazo zinachukuliwa kama ni tabia zisizokubalika ndani ya harakati za Wikimedia:
3.1 – Udhia
Hii ni pamoja na tabia yoyote ambayo kimsingi lengo lake ni kumtisha, kumtia hasira au kumkasirisha mtu. Tabia inaweza kuchukuliwa kuwa ni ya kiunyanyasaji iwapo inavuka mpaka wa kawaida ambao mtu yeyote wa kawaida angetegemewa kuvumilia (huku hali ya kitamaduni ya watu husika ikizingatiwa ). Unyanyasaji mara nyingi huchukua hali ya uumizaji wa hisia, hususani kwa watu walio katika mazingira magumu.
- Matusi: Hii inahusisha uitanaji wa majina yasiyofaa, kupiga vijembe au ubaguzi, au mashambulizi yoyote yanayojikita katika kuongelea kwa ubaya sifa za mtu binafsi. Matusi yanaweza kulenga sifa za mambo kama vile akili, muonekano, kabila, rangi, dini, ulemavu, umri, utaifa, ushiriki wa kisiasa, au sifa zingine. Kwa muda mwingine, matani ya kurudia rudia, kejeli, au uchokozi vinaweza kuchukuliwa kama matusi kwa pamoja, hata kama matamko pekee katika umoja wake yasingeonekana kuwa tusi au matusi.
- Unyanyasaji wa kijinsia: Kumtengenezea mtu dhana ya kimapenzi au utoaji wa kitu chochote kwa watu wengine kwa lengo la kupata malipo ya kimapenzi.
- Vitisho:' Kutumia uwezekano wa unyanyasaji wa mwili, hatua za kisheria, fedheha isiyo ya haki, au kuchafua sifa ya mwingine ili kushinda hoja au kulazimisha mtu aenende kama utakavyo wewe.
- Kuhamasisha madhara kwa wengine: Hii inahusisha kumshawishi mtu mwingine ajidhuru au ajiue vilevile kumshawishi mtu mwingine afanye madhara fulani kwa mtu mwingine.
- Udukuzi wa taarifa binafsi: Hii inahusisha kuchapisha taarifa binafsi za watu wengine, kama vile jina, mahali, sehemu aliyoajiriwa, anuani au barua pepe, bila kuwa na idhini ya mhusika. Kiwango cha kimsingi kabisa kilichowekwa katika mwongozo huu ni kwamba mtu hatakiwi kamwe kuchapisha taarifa za mtu ambazo mtu huyo (mlengwa) amejaribu kuzifanya siri/binafsi zisichapishwe mtandaoni. Jumuiya zitakuwa na viwango vikubwa zaidi ya hiki na wanaweza kupendelea kuzuia uchapishwaji wa taarifa zilizoko kwingineko mtandaoni lakini hazijawekwa katika miradi ya Wikimedia na mhusika mwenyewe.
- Ufuatiliaji: Kumfuatilia mtu katika mradi na kukosoa kazi zake kwa kurudia rudia kwa lengo la kumkasirisha au kumvunja moyo.
- Ukatishaji wa mazungumzo: Uharibifu/ukatishaji wa makusudi wa mazungumzo ya watu au kuchapisha kitu kwa nia ovu ya kutaka kumchokoza mtu fulani.
3.2 – Matumizi mabaya ya madaraka, haki, au ushawishi
Matumizi mabaya ya madaraka hutokea pale ambapo mtu mwenye wadhifa, hadhi au ushawishi fulani anajihusisha katika tabia isiyo na heshima, ukatili na vurugu kwa watu wengine. Katika mazingira ya Wikimedia mara nyingi inahusisha hali ya unyanyasaji wa kihisia (matusi, unyanyasaji wa kifikra, unyanyasaji wa kisaikolojia) na pia matumizi mabaya ya madaraka yanaweza kuingiliana na dhana ya unyanyasaji kwa ujumla.
- Matumizi mabaya ya madaraka kwa watendaji, viongozi na wafanyakazi: Matumizi mabaya ya mamlaka, ujuzi au rasilimali wanazopewa watendaji wa miradi, pia kwa viongozi na wafanyakazi wa Wikimedia Foundation au Washirika wa Wikimedia kuwatisha au kuwaogopesha wengine, au kwa faida zao binafsi za vitu au zisizo za vitu.
- Matumizi mabaya ya ukuu na kujuana: Hali ya mtu kutumia cheo chake na wadhifa wake kuwatishia wengine. Tunawaomba watu wenye uzoefu mkubwa na wenye kujuana na watu wengi katika harakati za Wikimedia kujiheshimu kwa makini kwasababu maoni ya uhasama yanaweza kubeba athari isiyokusudiwa ya kuunda vitisho kutoka kwa marafiki na wafuasi.
- Ulagahai wa Kisaikolojia:Kitendo cha mtu/kikundi cha watu kufanya kitu fulani ili kumfanya mtu/watu watilie shaka maoni yao binafsi, akili zao, au uelewa wao. Watu wenye mamlaka ya kijamii wana fursa maalum ya kutazamwa kama watu waaminifu, na hawapaswi kutumia vibaya nafasi hii kuwashambulia wengine ambao hawakubaliani nao.
3.3 - Wizi wa maudhui na matumizi mabaya ya miradi
Kuingiza taarifa zisizo sahihi kwa makusudi au taarifa zenye kuegamia upande mmoja katika miradi ya Wikimedia au kuzuia utengenezaji wa maudhui. Hii ni pamoja na; (na vingine ambavyo havijatajwa hapa, lakini vinafanana na hivi vilivyoelezewa hapa chini)
- Tabia ya kuondoa maudhui ya Wikimedia bila ukaguzi yakinifu kutoka kwa kundi la wakaguzi wa maudhui au uondoaji wa maoni/mrejesho mzuri wenye lengo la kujenga.
- Kuufanya mfumo uendeshe maudhui kwa namna ambayo mfumo huo utapindisha au kupendelea tafsiri ya ukweli au mtazamo fulani.
- Kauli za chuki za aina yoyote, au lugha ya ubaguzi, zenye lengo la kudharau, kudhalilisha, au kuchochea chuki dhidi ya kikundi au tabaka la watu kwa misingi ya rangi, dini, rangi ya ngozi, utambulisho wa kijinsia, mwelekeo wa kijinsia, kabila, ulemavu, au asili ya utaifa
- Uongezaji wa alama, picha, au maudhui usiokuwa na sababu na usio na uthibitisho kwa nia ya wengine.